WATAALAMU wa tafiti za
mazao ya kilimo na chakula nchini wameshauriwa kuendelea kufanya tafizi
za mazao mbalimbali ili kusaidia upatikanaji wa mbegu bora lengo likiwa
ni kumkomboa mkulima aweze kupata mavuno mengi.
Ushauri huo umetolewa
na mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Hamza Mahamud mara baada ya kukagua
shamba la mfano lenye ukubwa wa ekari tatu za muhogo aina ya kiroba
lililopo kwenye kijiji cha Gombero wilayani Mkinga hapo jana.
Alisema kuwa mbegu hiyo
licha ya kuwa ya majaribio lakini tayari imeanza kuonyesha matokeo bora
katika maeneo mbalimbali ilipopandwa hali inayotoa matumaini kuwa aina
hiyo ya mbegu ni mkombozi wa mkulima wa muhogo hapa nchini.
"Nawahimiza wakulima
wote nchini endeleeni kulima kilimo chenye tija kwa kuhakikisha mnapata
mbegu bora, pembejeo bora pamoja na kupanda kwa wakati huku mkifuatilia
kwa ukaribu ushauri wa wataalamu wetu,"alisema Mahamud.
Vile vile aliwaomba
wataalamu hao kuhakikisha wanapata tiba ya magonjwa ya mazao hayo pamoja
na kuwashauri wakulima njia bora za kilimo kwa lengo la kumkomboa
mkulima hasa wa kijijini kwani maisha yao yote yanategemea kilimo.
Nae msimamizi wa shamba
hilo Lucy Yohana alisema kuwa shamba la mfano hilo limeweza kutumia
kiasi cha sh. milioni 2.6 toka maandalizi ya shamba hadi palizi nne
ambapo wanatarajia kupata mbegu milioni 49 baada ya mavuno ya kwanza
ambazo zitaweza kusambazwa kwa wakulima wilayani humo.
Hata hivyo alisema kuwa
changamoto kubwa wanayoipata sasa ni mbegu hiyo kuanza kushambuliwa na
ugonjwa wa batobato hali ambayo imesababisha kuharibu zao hilo, kwa
kipindi cha miezi mitano zaidi ya mashina 40 mpaka sasa yameharibika
toka kupandwa.
Jambo jingine lililozungumzwa na Mahamud ni kuwaomba Watanzania kuendelea kuitunza tunu ya amani iliyopo nchini
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment