Wednesday, July 2, 2014

viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa katavi hatimae wamejiondoa rasmi katika chama hicho na kwenda chama cha ACT Allince for change and Transparency

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 
Walter mguluchuma
katavi


viongozi  wa  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo  chadema  mkoa wa  katavi  hatimae  wamejiondoa  rasmi  katika  chama  hicho  na  kwenda  chama  cha  ACT  Allince for  change  and  Transparency  ambacho  kinakuja  kwa  kasi  kubwa  hasa  mikoa  ya  ukanda  wa  ziwa  Tanganyika.
Akizungumza  na  waandishi  wa  habari wa  mtandao  huu  Joseph  Mona  ambae alikuwa  katibu  wa  chama  hicho  mpanda mjini alisema  kuwa  kumekuwa  na sintofahamu  ya  muda  mrefu  ndani  ya  chama  hicho  hatua mbayo  imewafanya  wao  kujiengua  richa  ya  baadhi  ya  viongozi  wao  kusimamishwa  uongozi  akiwa aliekuwa  mwenyekiti  wa  chama mkoa  Mzee  John  Malaki

Ata hivyo Mona    amesema chanzo  cha  malumbano  ndani  ya  chama  hicho  kimetokana  na  baadhi  ya  viongozi  wa  kitaifa kutowajali  wanachama  na  uongozi uliokuwa  madarakani  uku  wakiwatuhumu baadhi  ya  viongozi na  mbunge  wa  chama  hicho  jimbo  la  mpanda  Said Amour Arfi kuwa  walitumiwa na ccm  kuacha  nafasi  wazi  ya  jimbo  la mlele na  kumuachia  kupita  bila  kupingwa mh waziri  mkuu  mizengo  Pinda  maarufu  kama mtoto  wa mkulima uku wakidai  mbunge  wa  chama  hicho  hausiki  kwa  namna  yoyote juu  ya suala hilo.

viongozi  hao  waliotoka madarakani wamekituhumu  chama  hicho  kutotoa  fedha za  ruzuku  kwa  wakati  ama  kutotoa  kabisa  na  kukifanya  chama  hicho  kutojiendesha chenyewe

Alisema  pia  kumekuwa  na  matumizi  mabaya ya  fedha  ndani  ya  chama  hicho  uku  kikao  cha  mawasiliano  ndani  ya  mkoa  kikifumbia  macho  hali  hiyo

Mona  amewataja  wanachama  waliofukuzwa  hapo  na  chama  hicho  ambao  sasa  wamejiengua  kabisa  kuwa  ni  pamoja  na  Cnraradi Sinkala(mwenyekiti  kata  ya  makanyagio) IDEPHONCE  KITUNDU (mwenyekiti  kata ya ilembo)YASINI LUDANGA (MWENYEKITI  KATA  YA nsemlwa, medadi  khalfan  katibu  kata  nsemlwa,Mohamed kazyoba mjumbe  kamati  tendaji jimbo,SEFU  JUMA mwenyekiti  wa  BAVICHA jimbo la  mpanda  mjini,Clispin Salya mjumbe  kamati  tendaji  jimbo,Ana Paulo mwenyekiti  wa  BAWACHA mkoa,Rukia Juma Mhasibu wilaya mpanda,

wengine  ni  Charles  mwenyekiti  kata  ya  Misungumilo,Beatrice  Baraga mwenyekiti  BAWACHA jimbo,GODI  KAPUFI mwenezi  jimbo mjini mpanda,joseph  mona  katibu  jimbo  mjini,Sefu Said Spia mwenyekiti  jimbo  la  mpanda  na  aliekiuwa  mwenyekiti  wa  mkoa  Jonh  Malaki ambao  wote hawa  walifukuzwa ndani  ya  chama  kwasababu  ya  kuhoji  na  kufatilia  matumizi  ya  pesa  za uendeshaji  wa  chama  hicho

ata  hivyo  wanadai  walifukuzwa  kupitia kikao cha Mashauriano  ya mkoa na  kusema  hakikuwa  kikao  halali  chenye  mamlaka  ya kufukuza  na  kusema  kikao  chenye  mamlaka  ya  kufukuza  kinidhamu ni  kikao  cha  baraza  la uongozi  mkoa

akijibu  hoja  hizo  kaimu  mwenyekiti wa  mkoa  ambae  pia  ni  mwenyekiti  wa  baraza  la  vijana  sasa  Mangweshi  anadai  viongozi  hao  walifukuzwa  kwa  sababu  ya  kuwa  mamalukli  wa  chama  cha  mapinduzi na  kusema  chadema itaendelea  na  kwamba  imeanza  na  mungu,ipo  na  mungu  na  itamaliza  na  Mungu  uku  akishangazwa  kuanzishwa  kwa  chama  hicho  kwa  kuwa  watu  wanataka  maendeleo  na  sio n vyama.

No comments:

Post a Comment