Wednesday, July 2, 2014

Mwanamke auwawa kwa kukatwa na mapanga huku Mkwewe akishudia‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter   Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Mwanamke mmoja  aliyefahamika kwa jina la Suzana  Kingi  (40) Mkazi wa Kijiji  cha  Mwamkuru  Wilaya ya Mpanda  Mkoani Katavi ameuwawa  kwa kukatwa katwa na  mapanga shingoni  kichwani na mikononi  na  watu wasiojulikana 
Tukio hilo la mauwaji ya kinyama yalitokea hapo juzi majira ya saa  tisa usiku nyumbani kwa marehemu kijini hapo  alipokuwa akiishi
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari siku hiyo ya tukio  marehemu alikuwa amelala  kwenye nyumba yake  akiwa peke yake  jirani  na nyumba waliokuwa wakiishi wakwe zake  Maria  Kayungiro na    Maria  Nsabi wake wa mtoto wake aitwaye  Paul  Charles
 Alisema wakati Maria  Kayungiro  akiwa chumbani  kwake amelala  alimsikia marehemu  akikimbia  toka kwenye  nyumba  aliyokuwa amelala  akielekea kwenye nyumba ya mtoto wake   Paulo  Charles  huku  akipiga  mayowe ya kuomba msaada  kuwa  anakufa
 Marehemu  alifika  kwenye nyumba hiyo  ya mwanae  na  aliweza  kusukuma mlango wa nyumba na kufanikiwa  kuingia  ndani hadi  chumbani  huku akiendelea  kupiga mayowe ya kuomba msaada
Kidavashari  alieleza  wakati huo muuwaji  alikuwa  akimfuata  kwa nyuma  na bahati mbaya mtoto wake  mwenye nyumba hiyo  akuwepo  alikuwa amekwenda kwenye harusi kijiji cha jirani  ndani ya nyumba alikuwemo  Maria  Nsabi
Alisema  ndipo muuwaji huyo  aliweza kuingia ndani  na kuanza kumkatakata marehemu  huku akiwa juu ya kitanda cha mwanae  wakati akiendelea  kutekeleza  mauwaji hayo  alikuwa  akimmulika  Maria  Nsabi  kwa tochi  huku  akimtishia  kuwa akipiga kelele  nae atamuuwa kama mama mkwe wake
Kidavashari alifafanua  ilipotimia majira ya saa kumi  usiku  Paulo Charles  alirejea nyumbani kwake kutokea harusini  aliingia ndani  na kumkuta mkewe  Maria  Nsabi  akiwa amekaa chini  kimya  na ndipo alipomuhoji  kulikoni
Kabla hajamjibu  aliangalia kitandani  na kumwona mama yake  akiwa anavuja damu  alipojaribu kumsehesha hakuweza kujibu  ndipo  alipoweza gundua kuwa mama yake ameisha uwawa
Kamanda Kidavashari alisema  ndipo Charles  alipotoa taarifa  kwa majirani  na kwenye uongozi wa Serikali ya jijiji   na kisha kwa jeshi la Polisi
Alisema uchunguzi wa awali  unaonyesha   chanzo  cha  mauwaji  hayo  yanahusishwa  na masuala ya kishirikina  na hakuna mtu wala watu walikamatwa kuhusiana na tukio hilo  na jeshi la polisi kwa kushirikiana  na wananchi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo

No comments:

Post a Comment