Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baraza la
Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mpanda
limeunda timu ya madiwani watano kwa ajiri ya kuchunguza fedha
kiasi cha shilingi milioni mia moja za fedha za maendeleo za msimu wa mwaka 2012 na 2013 zinazodaiwa
kutumika kwa matumizi ya mengine bila idhini ya madiwani
Kikao hicho cha dharula
cha Baraza la madiwani
kilifanyika hapo juzi katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo kilichoongozwa na makamu wa Halmashauri
hiyo Yusuph Ngasa
Baraza la
madiwani lililazimika kufanya kikao
hicho cha dharula kufutia Halmashauri hiyo kutakiwa kujibu hoja ya mkaguzi mkuu wa
hesabu za Serikali kuibaini Halmashauri hiyo kutumia zaidi ya shilingi milioni mia
moja fedha za miradi ya maendeleo katika msimu wa fedha wa mwaka 2012 na 2013
Katika kikao
hicho makamu mwenye kiti wa Halmashauri hiyo alilieleza baraza hilo la madiwani
kamati ya fedha uchumi na mipango iliyokutana kwa muda wa siku mbili
kupitia tuhuma za Halmashauri hiyo zilizotolewa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
ilibaini kuwepo kwa tatizo hilo la
watumishi wa Halmashauri hiyo kutumia
fedha kinyume na utaratibu
Diwani wa Kata ya
Ilembo Wensilausi Kaputa alitaka Baraza lipatiwe majina ya watumishi
ambao walihusika na huhamisha fedha hizo za miradi ya maendeleo kwa matumizi wakati
wakijua ni kinyume cha sheria
Alieleza inatia shaka hata fedha hizo unaweza ukakuta zilitumika kwa matumizi
yao binafsi hivyo ni vizuri wakachukuliwa hatua haraka
iwezekanavyo kwani tatizo hilo sio jipya kwa Halmashauri hiyo
Mwenyekiti wa kikao hicho Yusuph Ngasa aliwaeleza madiwani hao kuwa kikao hicho kwa mujibu wa taratibu
wa kazi za kiutumishi alina mamlaka ya kumwajibishi aliye kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kipindi hicho
Joseph Mchina ambae ndiye aliyeidhinisha
fedha hizo zitumike kwa matumizi mengine na kwasa yeye yuko
manispaa ya Singida
Alisema wao wanao
uwezo wa kuwachukuli hatua za kinidhamu
watumishi wengine wawili ambao wanatuhumiwa kuwahamisha fedha hizo
kinyume na utaratibu ambao ni mchumi wa Halmashauri Frednandi Filimbi na mweka hazina Juma
Luhomwa
Baada ya maelezo
hayo ya mwenyekiti wa kikao hicho wajumbe wa baraza la madiwani walifikia
uamuzi wa kuunda kamati ya madiwani
watano ambayo itafanya kazi ya
kuchunguza matumizi ya fedha hizo na
itaanza kazi leo na itaongozwa na makamu
mwenyekiti wa Halmashauri Yusuph Ngasa
na itafanya kazi kwa muda wa siku 14
N a
walikubaliana watumishi
haowawili wapewe adhabu za kiutumishi za kukiuka utaratibu wa kutumia fedha za miradi ya maendeleo kwa matumizi
mengine na kusababisha miradi kushindwa
kukamilika kwani kosa hilo la kuhamisha
fedha halihitaji kusubilia timu ya iliyoundwa
kitakacho subiliwa ni fedha wamezitumiaje
Aidha kwa
Mkurugenzi Mchina walipendekezaKatibu Tawala wa Mkoa wa Katavi amwandikie
katibu mkuu wa Tamisemi barua kuhusu
malalamiko
ya madiwani jinsi Mkurugenzi huyo alivyohamisha fedha za
miradi ya maendeleo kwa matumizi mengine bila idhini ya m
No comments:
Post a Comment