Wednesday, July 16, 2014

HATARI SANA: MAUWAJI YAKUTISHA YASHAMILI KATAVI


Na  Walter  Mguluchuma Mpanda- Katavi yetu

POLISI mkoani Katavi  linawashikia  mkazi wa kitongoji  cha Kalufweshi  katika  kijiji cha Kakese – Mwakajuni Emanuel John (45) na mkewe Neema Edson (30) wakihusishwa na kuuawa kwa kikatili kwa hawara  ya  mshtakiwa .

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Katavi , Focus Malengo  amemtaja  marehemu  kuwa Theodora Mwamba (37)aliyeuawa  kwa kucharanga kwa mapanga  kichwani , kifuani na mgongoni  akieleza  kuwa  chanzo chake ni wivu wa kimapenzi .

Akizungumza na  waandishi wa habari  ofisini  kwake , Kaimu Kamanda , Malengo  alidai kuwa  tukio  hilo  lilitokea  usiku wa kuamikia Julai 13 , mwaka huu  sasa sita usiku  katia kitonngoji  hicho  cha Kalufweshi.

Akisimulia  undani wa  mkasa  huu  aliouita wa kikatili , Kaimu Kamanda , Malengo  alidai kuwa  mwezi mmoja  kabla ya  kutokea kwa kisa hiki , Emanuel  na Theodora  waliamua  kuishi  kinyumba  baada  ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi  kwa muda mrefu.

Inadaiwa kuwa wakati  mshtakiwa  akiishi na mkewe wa ndoa Neema  pia  alikuwa  na  mahusiano hayo   ya kimapenzi  na Thedora  na  kuzaanje ya ndo  mtoto mmoja wa kie aitwae Lily ..

Kwa mujibu  wa Malengo  , Julai 12 mwaka  huu  wageni  wawili  wa kiume walifika  nyumbani kwa Theodora na  kuomba maji  ya kunywa  kisha wakaondoka  baada ya  kunywa maji hayo .

Anaeleza kuwa  usiku  wa manane , Julai 13 Emanuel  akiwa  amelalala  nyumba kwa ‘mpenzi’ wake Theodora  aligutushwa na  mwanga  wa tochi  uliokuwa  ukimulika  chumbani  walimolala  kupitia  dirishani .

Inadaiwa watu  hao  waliokuwa  wakimulika  mwanga wa tochi  chumbani  walimolala Theodara na Emanuel walisikika  wakijieleza kuwa  wao  walikuwa  wametoka  majimboni  na kwamba  walitaka  kujua  hapo  walipo  ni  nani anaeishi .

“Ndipo mshtakiwa alipowajibu  kuwa  ni nyumbani kwa mama Lily  ndipo  watu hao  waliokuwa  nje ya nyumba hiyo  walijieleza kuwa  walikuwa wametoka  machimbon na kwamba walikuwa  wamefuata madini ya dhahabu  kwa mama Lily “ anaeleza Kaimu Kamanda Malengo .

Aliongeza kuwa ndipo  walipofungua  kwa nguvu mlango  wa mbele  wa nyumba hiyo na kuingia  ndani  wakiwa na  silaha za jadi na kuanza kuwashabulia  kwa  kuwacharaza fimbo “Emanuel Na Theodora  walifanikiwa kuwaponyoka  wavamizi  hao  na  kila mmoja wao  kukimbia maeneo  tofauti  kusalimisha  maisha yao “ anabainisha .

Inadaiwa kuwa  mshtakiwa (Emanuel) baadae aliamua kurejea  nyumbani  kwa Theodora  na kukuta akiwa ameuawa kikatili  kwa kucharangwa na mapanga  mita  chache kutoka  nyumbani  kwake .

Mauwaji ya mwanamke huyo niyatatu kutokea kwa watu kuuwa kikatili  kwa kipindi cha wiki moja mauwaji mengine ya watu kuuwa kikatili yaliitokea katika vijiji vya Kamsanga , Vikonge 

No comments:

Post a Comment