Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi limemchagua Juma Hawazi Ibrahimu ambae ni Diwani wa Kata ya Mwese kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kipindi cha kuanzia Julai 2014 hadi June 2015 Huchaguzi huo wa kumchagua Makamu mwenyekiti wa Halmashaurri hiyo ulifanyika hapo jana katika ukumbi wa Idara ya Maji ulioko mjini hapa Kikao hicho cha Baraza la madiwani kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kibeliti ambae pia ni Diwani wa Kata ya Mishamo Katika uchaguzi huo wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda nafasi hiyo ilikuwa na mgombea mmoja na alipigiwa kura za siri Makamu mwenyekiti huyo alichaguliwa kwa kupata kura 13 katika ya kura zote zilizopigwa ambapo kura zilizopigwa zilikuwa ni 13 na hakukuwa na kura hata moja iliyoharibika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda inajumla ya Madiwani kumi wa kuchaguliwa na waviti maalumu watatu na Mbunge mmoja Baraza hilo la Madiwani pia liliwachagua wajumbe na wenyeviti mbalimbali wa kamati watakao ongoza kwa pindi cha mwaka mmoja cha kuanzia julai 2014 hadi june 2015 mwakani

No comments:
Post a Comment