Saturday, July 12, 2014
Madiwani wa muagiza mkurugenzi kuhakikisha watendaji wa Vijiji wanaitisha mikutano mikuu
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda limemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Estomihn Changa’aha kuhakikisha watendaji wa vijiji wanafanya mikutano mikuu kwenye vijiji vyao na kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi
Madiwani wa Halmashauri hiyo walitoa agizo hilo hapo jana kufutia malalamiko ya baadhi ya madiwani walioyatowa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa kipindi cha mwaka 2013 na 2014 ulifanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Maji mjini hapa uliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kibiriti
Diwani wa Kata ya Kabungu Nassoro Kasonso ndiye aliyekuwa wa kwanza kutowa malalamiko kwenye baraza hilo ambapo alilamikia kitendo cha watendaji wa vijiji kutoitisha mikutano mikuu ya Vijiji na mikutano ya Halmashauri kuu za vijiji kwenye maeneo yao kulingana na taratibu za ratiba ya mikutano hiyo inavyoelekeza
Alisema watendaji hao wamekuwa hawaitishi mikutano kwenye vijiji vyao na badala yake wamekuwa wakiandaa mihtasari ya uongo na kuipeleka kwenye ofisi ya Mkurugenzi ilikuonyesha kuwa wanafanya mikutano kwenye vijiji vyao wakati sio kweli
Alifafanua watendaji hao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wenyeviti wa vijiji kugushi mihtasari hiyo kwa kutumia mihtasari ya vikao vilivyopita
Nae Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo Hamad Mapengo alieleza kuwa watendaji wa vijiji wamekuwa wakishindwa kuitisha mikutano mikuu kwa kuhofia kutoa taarifa za mapato na matumizi
Alisema watendaji wengi wa vijiji wamekuwa ni wabadilifu hivyo wamekuwa na wasiwasi wa kuulizwa maswali na wananchi kwenye mikutano mikuu ambao wengi wa wananchi huwa wanapenda kujua hari halisi ya mapato kwenye vijiji vyao
Alieleza vipo baadhi ya vijiji vinashindwa kufanya mikutano mikuu kutokana na vijiji hivyo kutokuwa na watendaji wa vijiji na kukuta mtendaji mmoja akawa pia anakaimu nafasi hiyo kwenye vijiji vingine
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Karema Michael Kapata alieleza kuwa sababu nyingine inayochangia watendaji wa vijiji na wenyeviti wao kuogopa kuitisha mikutano ni kuhofia kuhojiwa na wananchi kuhusiana na tabia yao ya kuuza adhi za vijiji kiholela na hasa kwa wafugaji wa mifugo
Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa na tabia ya kuuza adhi za vijiji bila idhini ya mikutano mikuu ya vijiji na kwenye maeneo ya hifadhi za mistu hivyo wamekuwa wakihofu kuhojiwa na wananchi kwenye mikutano .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estohn Chang’ah aliwaeleza madiwani hao kuwa tayari ameisha anza kuwachukulia hatua mbalimbali baadhi ya watendaji wa vijiji ambao wameshindwa kuwasilisha mihtasari ya mikutano mikuu ya vijiji vyao
Chang’ah alitaja baadhi ya hatua alizowachukulia watendaji hao ni kuwasimashia mishahara yao mpaka hapo watakapo kuwa wamewasilisha mihtasari kwenye ofisi yake na zoezi hilo ni la kudumu katika halmashauri yake
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Yassin Kibiriti aliwaeleza madiwani kuwa wanao wajibu kwenye maeneo yao kuhakikisha wanawasimia watendaji wa vijiji nakuhakikisha wanaitisha mikutano mikuu kwenye vijiji vilivyoko kwenye kata zao
Alisema kama mikutano haifanyiki matokeo yake inakuwa ni vigumu kwa wananchi kufahamu na kutambua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Halmashauri hiyo
Pia alikemea tabia ya viongozi wa vijiji na vitongoji kuacha tabia ya kukutana pale tuu wanapojua asilimia 20 ya fedha za mapato zinapo kuwa zimepelekwa na Halmashauri kwenye maeneo yao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:
Post a Comment