Monday, July 14, 2014
Halmashari Mpanda kuanzisha jumuia za watumiaji wa maji
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kupitia Idara yake ya Maji imepanga kuanzisha jumuia za watumiaji wa maji katika vijiji mbalimbali vya Halmashauri hiyo
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomhn Chang’ah wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa idara ya maji
Alisema Halmashauri hiyo kwa kutumia kitengo cha idara ya maji imepanga kuanzisha jumuia za watumiaji wa maji katika vijiji mbalimbali
Chang’ah alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Igagala, Ngomalusambo, Majalila , Kabungu , Kapalamsenga, Ikaka, Isenga Katuma na Mwese vijiji hivyo viko kwenye Tarafa za Karema , Kabungu na Mwese
Alisema uanzishwaji wa jumuia za watumiaji maji unatarajiwa kuanza kufanyika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2014 na 2015 kwa vijiji vya Ngomalusambo na Karema
Alifafanua idara ya maji katika Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbambali ambazo zimesababisha utekelezaji wa shughuli za miradi kuwa mgumu
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo wananchi kutotimiza michango ya ujenzi wa miundombinu mipya ya maji inayohitaji uchangiaji wa asilimia tano hasa katika uchimbaji wa visima virefu na vifupi,wananchi kuwa na mwamko mdogo wa uchangiaji
Changamoto nyingine ni kutopatikana kwa taarifa sahihi kutoka vijijini juuya uharibifu wa miundombinu ya maji kutoka kwa wananchi pamoja na Halmashauri kuletewa fedha kidogo kutoka derikali kuu kwa ajiri ya idara ya maji
Pia wananchi kuwa na dhana potofu ya kuwa miradi ya maji ni mali ya Serikali na wao wananchi hawahusiki hivyo kutokuwa na mwamko wa uchangiaji pamoja na wizi wa vipuri vya visima vinavyotumia pampu za mikono

No comments:
Post a Comment