Saturday, July 12, 2014
HATARI: MFANYABIASHARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI JICHONI
Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi,
MFANYABIASHARA mkazi wa kijiji cha Katuma wilayani Mpanda , Juma Luhanga (29) ameuawa kwa kupingwa risasi katika jicho lake la kushoto na watu wawili wanaosaidkiwa kuwa majambazi akiwa dukani kwake .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Focus Malengo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Julai 10 mwaka huu sa tatu na nujsu usiku kijijini Katumba maasrufu kwa uchimbaji wa dhahabu wilayani humo
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya siku , Kaimu Kamanda huyo wa Polisi , Malengo , watu wawili wamekamatwa wakihusushwa na mauaji hayo ambapo wanaendelea kushikiliwa na Polisi kwa mahojiano katia Kituo Kikuu cha Polisi kilichopo mjini Mpanda .
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Julius Charles Rajab (27)Mtaa wa Kashaulili na Keimark Emanuel Mwendapole (20)mkazi wa kitingoji cha Mjimwema mjini Mpanda.
Akisimulia mkasa huo Kaimu Kamanda Malengo alieleza kuwa usiku wa tukio hilo maremu alikuwa dukani kwake akiendelea na shughuli zake za kibiashara ambapo watoto wake watatu Vitus Luhanga (18) mkulima , Angelina Luhanga (14) na Leonard Dickson (12) wote wanasoma Shule ya Msingi Katuma walikuwa sebuleni wakiongea .
“Ghafla mmoja watuhumiwa hao alingia sebuleni na kuwaamuru watoto hao watatu kujisalimisha na kukabidhi fedha …. Ndipo baba yao aliposikia majibishano hayo na kwenda sebuleni na kukabiliana na mtuhumiwa huyo ambaye hakuwa na silaha yeyote na kufanikiwa kumtoa nje ya nyumba hiyo kisha akafunga mlango kwa ndani ……
Kisha akaenda dukani kwake ili kufunga dirisha la duka hilo “ anaeleza .
Inadaiwa wakati akijiandaa kufunga dirisha la duka hilo ndipo mmoja wa watuhumiwa hao alipomfyatulia marehemu risasi katika jicho lake la kushoto na kufa papo hapo .
Kwa mujibu wa Malengo watuhumiwa hao walifika eneo hilo la tukio wakiwa wamaevaa makoti marefu na nyuso zao zikiwa zimefunikwa ili wasiweze kubainika baada ya tukio hilo waliondoka wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya SunLG ambayo namba zake za usajiri hazikuweza kufahamiaka mara moja .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:
Post a Comment