Home » » FUSO LAUWA WAWILI NA KUJERUHI 32

FUSO LAUWA WAWILI NA KUJERUHI 32

Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.




Na Walter  Mguluchuma
Mpanda-  Katavi yetu Blog

WATU wawili  wamekufa papo hapo  na wengine 32 wamejeruhiwa  vibaya  huku mmoja wao akiwa amevunjika  miguu yote miwili baada ya gari  walilokuwa  wakisafiria  kuacha njia na kupinduka .

Ajali hiyo ya  barabarani  ilitokea  katika miteremko ya Mlima Sijonga  katika  barabara inayounganisha  Mji wa Mpanda  na Kijiji cha Karema  mwambao mwa Ziwa Tanganyika  wilayani Mpanda .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Focus  Malengo  akizungumza na mwandishi  wa habari  hizi  kwa njia ya simu  kutoka mjini Mpanda  amedai  ajali hiyo ilitokea   Ijumaa , saa nne usiku  katika Mlima Sijonga ikihusisha  gari aina  ya Fuso  yenye nambari za  usajiri T 759 FMU mali ya Ezekiel Molel (49) mkazi wa Mtaa wa Kawajense  mjini Mpanda .

Alimtaja mmoja  wa marehemu  kuwa  ni Hamadum Neema (34) mfanya  biashara  wa mjini Mpanda  ambapo mwingine  bado  hajatambuliwa  ila  anakisiwa kuwa na umri  kati ya  miaka 36 na 40.

Kwa mujibu  wa Malengo  gari hilo  lilikuwa  limebakia  wafanya biashara  na  likiwa  limesheheni  mizigo  mbalimbali ikiwemo  magunia  ya  mpunga  , mahindi na masanduku ya bia  na  vinywaji  baridi  likielekea  mjini Mpanda  likitokea  mnadani  kijijini Karema .

Kwa mujibu wa Malengo  dereva wa  gari  hilo  ambaye  ametambuliwa  kuwa Edwin Mgawe (37)  mkazi wa mjini Mpanda  anatafutwa na Polisi  ambapo alifanikiwa kutoroka  mara  baada ya kutokea kwa ajali hiyo .

“Uchuguzi wa awali umebainisha kuwa  mwendo  kasi na uzembe  wa  dereva  ndio hasa chanzo cha ajali hiyo “ alibainisha ,

Kwa mujibu  wa mganga Mkuu  wa Mkoa  wa Katavi , Dk Joseph Msemwa  amedai  kuwa  majeruhi wote  32   miongoni  mwao  wanawake  ni kumi na 22 wakiwa  wanaume  wamelalazwa katika Hospitali ya Wilaya  ya Mpanda  kwa matibabu .

“Hali za majeruhi  zinaendelea  vizuri  isipokuwa Hans Feso mwenye umri  wa miaka 32  hali yake  bado ni tete  ambapo  amekatika miguu yake  yote  miwili ….Pia miili ya marehemu  wawili  imehifadhiwa katika  chumba  cha kuhifadhia  maiti hospitalini hapa”  anabainisha Dk Msemwa .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa