Home » » POLISI WAVUNJA MKUTANO WA UKAWA

POLISI WAVUNJA MKUTANO WA UKAWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
JESHI la Polisi jana limevunja mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa madai kuwa wanasambaza CD za uchochezi.
Kuvunjwa kwa mkutano huo kunatokana na askari zaidi ya 20 waliokuwa kwenye gari mbili na moja la kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuanza kuwakamata walinzi wa viongozi wa UKAWA.
Vurugu hizo zilianza kutokana na Mjumbe wa Baraza Kuu Chama cha Wananchi (CUF) Joran Bashange, kuhutubia mkutano huo.
Wakati akihutubia, Bashange alisema kuwa katiba mpya haiwezi kupatikana kwa kuwa viongozi wengi ni mafisadi na pia Rais Jakaya Kikwete kuwa kigeugeu, na kwamba ametishwa na wana CCM kwenye makundi ya kugombea urais.
“Iwapo katiba mpya itapitishwa wengi wa wana CCM ambao ni mafisadi watapata hukumu na watafunguliwa mashitaka.
“Jeshi la Polisi limekuwa kibaraka wa Serikali ya CCM na ndiyo maana wameshindwa kuwakamata mafisadi na majambazi sugu na badala yake wamekuwa wakiwakamata vibaka na wezi wa simu,” alisema.
Alihoji kama Rais Kikwete ni kiongozi wa usawa kwanini ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi wanaoficha pesa nje na matokeo yake amekuwa akiwapandisha vyeo watuhumiwa hao.
Kauli hizo ziliwafanya polisi waingilie kati kwa kuwataka viongozi wa UKAWA wasiendelee na mkutano huo jambo lililopingwa na viongozi waliokuwa jukwani huku wakilindwa na walinzi wao.
Polisi walilazimika kupambana na walinzi na viongozi wa UKAWA hali iliyosababisha vurugu kubwa na kuvunjika kwa mkutano huo.
Mara baada ya tukio hilo viongozi wa UKAWA walilazimika kuvunja mkutano na askari kuwalazimisha walinzi wa viongozi hao kwenda katika kituo cha polisi.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa