Thursday, May 1, 2014

HATARI: ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUWA MKEWE KWA KIPINGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda  Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi   wa  Mkoa  wa Katavi  linamshikilia   Vitus   Mlengo  (22) Mkazi wa Kijiji  cha Manga  Kata ya Kasokola Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  kwa tuhuma  za kumsababishia kifo mke  wake  aitwaye   Aghata  Izack  (19) baada ya kumpiga akishirikiana na   Faustina Matheo (31 kwa madai  kuwa marehemu mkewe alikuwa ni mvivu  wa kufanya kazi za shambani na nyumbani
Kwa mujibu  wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Katavi  Kamishina  msaidizi  Mwandamizi  Dhahiri Kidavashari  alisema chanzo  cha kifo cha mwanamke  huyo ni  ugomvi baina ya wanandoa hao wawili  ulitokea  hapo   Aprili  25  mwaka huu majira ya saa sita  mchana  nyumbani kwao kijijni  hapo

Alisema  marehemu  ambae   alikuwa ni mjamzito  siku  iliyofuata  aliamka  akiwa anajisikia vibaya  kutokana na kipigo  aliamua  kwenda  kwenye zahanati ya Kasokola  iliakafanyiwe uchuguzi na kupatiwa matibabu  lakini  kabla  ya kufika  kwenye Zahanati  alipitia kwa mama yake  mdogo aitwaye   Anastazia Charles  na ndipo  alipomweleza  kwamba anajisikia  vibaya  kutokana  na kipigo  alichopigwa na mume wake  aliyeshirikiana na  Faustina  Matheo  kumpiga yeye
Alifafanua  baada ya kupata tiba kwenye zahanati hiyo  wakati anarudi nyumbani alipitia  nyumbani kwa bibi yake  aitwaye  Lucia  Ramadhani  na kumsimulia  kuhusu kupigwa kwake  pia alimweleza  kwamba mumewe   alimwambia marehemu  asirudi  nyumbani  bila  mboga  hivyo bibi yake alimmpatia mboga  ya kwenda nayo  nyumbai kwa mume wake 

Alisema Marehemu  alipofika nyumbani  mume wake  alimfukuza  na hatimae aliamua  kurudi  kwa bibi yake   na kulala  hapo hadi kesho yake  majira ya asubuhi  aliporudi  kwa mumewe ambae alikubali kumpokea  na wakaendelea  kuishi kama kawaida 

Alieleza   siku ya tarehe  28  majira ya saa mbili usiku  marehemu aliandaa chakula  cha usiku  lakini alishindwa kula  kutokana na kujisikia vibaya kiafya   na matokeo yake alianza kutapika huku akiwa analalamika kuwa anasikia mwili unamuuma  pamoja na kichwa  na ghafla hari ikabadilika  na kuwa mbaya  hari ambayo ilimfanya mume wake  aombe msaada kwa jirani yake aitwaye   Alfred  Kasonso  na  walijitahidi  kumpa huduma  ya kwanza  lakini hari ilizidi kuwa mbaya 

Kidavashari aliesema baada ya kuona hari inazidi  kuwa mbaya  walitafuta usafiri wa pikipiki  kwa lengo la kumuwahisha katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa matibabu  lakini wakati wakiwa njia  kabla ya kufika  hospitali  alifariki Dunia 

Alisema mume wa marehemu  na Fausti  Mathew wanashikiwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi  na endapo   itabainika  kwamba wao ndio waliohusik  na  kifo cha marehemu  watafikishwa  kwenye vyombo   vya sheria

No comments:

Post a Comment