Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Askofu Gervas Nyaisonga (48 )anasimikwa kesho siku
ya jumapili kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda katika ibada inayotarajiw kufanyika kuanzia
saa nne asubuhi katika viwanja vya shule ya chekechea inayomilikiwa
na Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda
kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa na uongozi wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda ibada ya kusimikwa Askofu Nyaisonga itahudhuriwa na Maaskofu wote wa Kanis hilo na mapadri
watawa na walei wakutoka majimbo mbalimbali ya kanisa hilo
Askofu Nyaisonga anahamia jimbo Katoliki la Mpanda kabla ya hapo alikuwa ni Askofu wa
Jimbo la Dodoma jimbo la Mpanda lilikuwa halina Askofu toka
mwaka juzi kufuatia kufariki kwa
aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo Paskal Kikoti
kufariki Dunia hapo mwaka juzi
Jimbo Katoliki la
Mpanda lilianzishwa mwaka 2001 na Askofu wake wa kwanza wa Jimbo hilo alikuwa
ni marehemu Paskali Kikoti hinyo Askofu
Gervas Nyaisonga atakuwa ni Askofu wa PILI tangia jimbo katoliki la Mpanda
lilipoanzishwa
Katika ibada hiyo
ya kusimikwa kwa Askofu Nyaisonga Serikari itawakilishwa na Waziri wa Nchi
ofisi ya waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshaji Mery Nangu ambae
atatowa salamu za Serikali kwenye ibada hiyo
Miongoni wa
watakao hudhuria ibada hiyo hapo kesho
ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na viongozi mbalimbali wa Serikali wa
Mkoa wa Katavi na Viongozi wa mikoa ya jirani ya Rukwa Tabora na Kigoma
No comments:
Post a Comment