Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATU wanane wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za
jadi, wamevamia kambi ya kampuni ya Wachina wanaotengeneza
barabara ya kiwango cha lami kutoka Mpanda hadi Sitalikei, wilayani
Mlele na kumjeruhi mlinzi wa kampuni hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Dhahiri Kidavashari, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22, saa 5
usiku katika kambi hiyo iliyopo Kata ya Magamba.
Alisema watu hao baada ya kufika kwenye kambi hiyo walimvamia
mlinzi, Joseph Sarangi na kumshambulia kwa mapanga na marungu na
kumjeruhi kwenye paji la uso na kichwani na kufanikiwa kuiba
betri ya gari.
Kidavashari alisema muda mfupi baada ya tukio hilo, askari walipata
taarifa na kuanza kuwafuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni
mtuhumiwa, Juma Athumani (23), mkazi wa Mtaa wa Tambukareli mjini
hapa.
Alisema polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine saba ambao walishiriki tukio hilo.
Chanzo:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment