Home » » CHADEMA KATAVI WAPITISHA UAMUZI WA KUWATIMUA VIONGOZI WAO NA KUSIMAMISHWA KWA MWENYEKITI WA MKOA NA MADIWANI 2 KUSUBIRIA MAAMUZI YA KAMATI KUU‏

CHADEMA KATAVI WAPITISHA UAMUZI WA KUWATIMUA VIONGOZI WAO NA KUSIMAMISHWA KWA MWENYEKITI WA MKOA NA MADIWANI 2 KUSUBIRIA MAAMUZI YA KAMATI KUU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamiko@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
Mkuutano  Mkuu wa Mkoa  wa  Katavi  wa    Chama   cha   Chadema  umepitisha  uamuzi  wa  kuwavua  yadhifa   viongozi  wa chama  hicho wa  Jimbo  la Mpanda  Mjini  na  kumsimamisha  mwenyekiti wao wa Mkoa huu John Malack na kutuma    mapendekezo kwenye  kamati kuu ya Taifa ya  chama  hicho  mapendekezo ya  kuwavua  uanachama  madiwani wake  waili  wa Kata ya Makanyagio na Kashaululi
Wajumbe  wa Mkutano huo  mkuu  wa Mkoa  wa  Katavi  walipitisha  maazimio hayo   hapo juzi  kwenye  mkutano  uliofanyika kwenye  ukumbi wa Mtakatifu Maria  wa Kanisa  Katoriki Jimbo la  Mpanda na uliongozwa  na Makamu  mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Magharibi    Masanja  Mussa Katambi
Viongozi  hao  wameodholewa    nyadhifa  zao  kutokana  na  tuhuma  za kuwatolea  kashifa  viongozi wao wa Taifa kwenye  mkutano  wao wa hadhara  uliofanyika  februali 2 kwenye   viwanja  vya Maridadi Mjini  hapa
Viongozi walioondolewa  kwenye   nyadhifa  hizo  ni Mwenyekiti wa Jimbo  la Mpanda Mjini Seif  Sipia   Katibu wa  Jimbo  hilo   joseph  Mona   katibu   mwenezi  Godfrey Kapufi  ambae wamemvua  uanachama  kutokana  na  kudaiwa  kuiba  nyaraka ya  Chama   hiyo na kuisoma  kwenye  Mkutano  huo wa  hadhara
Pia  wajumbe wa Mkutano  mkuu  huo  walipitisha  uamuzi  uliotolewa  na    kikao cha  mashauriano  cha  Mkoa  kilichoketi  tarehe 22    Februari na kutowa uamuzi   wa kumsimaisha  mwenyekiti wao wa  Mkoa wa Katavi  John Malack  kwa  tuhuma za  kushiriki kwenye  mkutano huo   ambao  yeye  ndiye  aliyefunga  mkutano huo wa  hadhara
  Katibu  wa Mkoa  wa  Chama  hicho   Almasi   Ntije  aliwaeleza  wajumbe wa  Chama  hicho  kuwa  mwenyekiti huyo wa  Mkoa  ataendelea  kusimamishwa  kufanya  shughuli za   chama  hicho  hadi hapo  utakapo tolewa  uamuzi juu yake  na  kikao cha  kamati kuu abacho  ndicho  chenye  mamlaka
 A lisema  kwa  upande  wa  madiwani  wakata ya   Makanyagio  Iddi Nziguye na  Diwani  wa  Kata ya  Kashaulili  John  Matongo  nao mapendekezo yao ya  kuwavua  uanachama   yameisha pelekwa  kwenye  kamati kuu ya  chama hicho  na  ndicho kikao chenye  mamlaka  nayo
Kwa  upandea  wake   Diwani wa  Kata ya  makanyagio   Iddi  Nziguye  alipohojiwa  na mwandishi wa  habari  hizo  kuhusiana na uamuzi wa  mkutano mkuu huo  alisema  kikao hicho  hakikuwa  harali kwani  kilikuwa  na  wajumbe  ambao  sio wajumbe  wa kikao hicho
Alifafanua  kuwa  idadi ya wajumbe walioshiriki  mkutano huo walikuwa zaidi ya  mia tatu wakati wajumbe  harali wa  mkutano huo  huwa  hako  zaidi ya  mia  na  hamsini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa