Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAVUVI wawili wilayani Mlele, Katavi wameuawa kwa kupigwa
risasi na askari wa Game Reserve walipokuwa wakivua samaki ndani ya
Hifadhi ya Pori la Akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa kwa
risasi.
Waliouawa wametajwa kuwa ni James Mauto (21), mkazi wa Kijiji
cha Ugala na January Marekani (18), Mkazi wa Kijiji cha
Mtapenda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema
jana kuwa tukio hilo lilitokea Februari 28, mwaka huu, saa tisa
alasiri ndani ya Hifadhi ya Pori la Akiba la Ugala.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment