Home » » DC AMPA SIKU SABA MWANDISI WA UJENZI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA JENGO NA KUSABABISHA KUJENGWA CHINI YA KIWANGO‏

DC AMPA SIKU SABA MWANDISI WA UJENZI KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA JENGO NA KUSABABISHA KUJENGWA CHINI YA KIWANGO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amempa  siku saba Mwandishi  wa ujenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda  Albati Kinyando  kuhakikisha jengo la Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Misunkumilo  Wilayani hapa lililojengwa chini ya kiwango kutokana na usimamizi mbovu wa Idara ya Ujenzi  linafanyiwa marekebisho
Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda  alitowa agizo hilo hapo juzi wakati wa ziara yake  alipotembelea  kata hiyo ya Misunkumilo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya   maendeleo
Mwamlima alishitushwa  na ujenzi wa jengo hilo  ambalo ni jipya  lilijengwa na Kampuni ya Kitu Kizima ya Mjini hapa  mara   baada ya kuingia ndani ya ofisi hiyo na kukuta  kuta za jengo hilo ambalo ni jipya kabisa  likiwa kuta zake  zikiwa   zimepasuka na milango ya jengo ikiwa imepinda  na baadhi ya vyumba  vikiwa havina mirando
Kabla ya kutowa agizo hilo kwa Mwandisi  wa Ujenzi  Mkuu wa Wilaya ambae pia alikuwa amefuatana na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda  alipokea taarifa  ya ujenzi wa jengo  la ofisi hiyo iliyosomwa na Afisa    M tendaji wa Kata hiyo January Kajungilo
Afisa Mtendaji alieleza  kwenye taarifa  kuwa jengo ujenzi wa jengo   ujenzi wake  megharimu  jumla ya shilingi milioni 28,630,417 kati ya fedha hizo nguvu ya wananchi walichangia  NI Shilingi milioni  4,126,000 na Halmashauri ya Mji  wa Mpanda ilitowa shilingi milioni  24,516,417
Alisema ujenzi  wa jengo hilo ambao ulujengwa na Kampuni ya Kitu  Kizima Contacter  ya  mjini Mpanda ulianza kujengwa  mwezi mei  2012 na jengo hilo  lilipaswa kukamilika mwezi Novemba mwaka 2012
Alifafanua  jengo hilo  ambalo halijaanza kutumika  limekabidhiwa hivi karibuni  huku mkandarasi akiwa  amebaki anadai  shilingi  526,000 kati ya fedha zote
Kwa upande wake Mwandisi wa ujenzi Albati Kiyando alimweleza Mkuu wa Wilaya  kuwa atatekeleza agizo hilo kwa  kushughulikia  marekebisho ya jengo hilo la Afisa Mtebdaji wa kata kwa kulifanyia marekebisho sehemu zote  zinazostahili  kufanyiwa marekebisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa