Home » » RC KATAVI AWATAKA VIONGOZI WA HALMASHAURI KUEPUKA MIGONGANO YAO ISIYO NA LAZIMA BAINA YAO NA WAALIMU‏

RC KATAVI AWATAKA VIONGOZI WA HALMASHAURI KUEPUKA MIGONGANO YAO ISIYO NA LAZIMA BAINA YAO NA WAALIMU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR   Rajabu Rutenwe  ameziagiza Halmashauri  zote za Mkoa wa Katavi  kuhakikisha  zinaondoo migogoro yote   isiyokuwa na  sababubaina   ya waalimu  na  viongozi wa  Elimu wa Wilaya  na baina ya Wakurugenzi na  waalimu
Kauli hiyo ya agizo alitowa hapo juzi wakati akifungua   kikao  cha kazi  kilichowashirikisha  viongozi  wa elimu  kutoka Hamashauri zote  nne  za Mkoa wa Katavi  na viongozi wao wa elimu wa mkoa kilichofanyika  kwenye ukumbi  wa Inyonga Wilayani Mlele
Dr Rutengwe alisema  anawaagiza viongozi wote  wa elimu  waakikishe wanawatendea haki waalimu  wote  na kwaharaka  wanapokuwa waalimu wamefika  kwenye ofisi zao  kwa ajiri ya shida mbalimbali
Alisema wapeni haki zao  mapema   bila kuwazungusha  na kama kunasababu  inayokwamisha  basi  wapeni majibu  mazuri yanayowatia matumaini  kwa waalimu
Alifafanua kuwa sio jambo jema  kuwakatisha tamaa waalimu  hasa kwa kutowajali  wanakwenda ofisini kwao  kwa ajiri ya kupata  ufumbuzi wa  shida zao mbalimbali  zinazokuwa zinawakabili
Mkuu wa Mkoa alieleza  kuwa yapo malalamiko  wanayolalamikiwa viongozi kuwa wamekuwa na tabia ya  kutowajali waalimu kwa kuwatolea  majibu  yasiyoridhisha  kuwakashifu  na kuwadharau waalimu  au kuwaonyesha ukubwa wao kwenye ofisi zao
Hivyo  ni vema tabia hiyo waiashe  na  wajirekebishe  kwa kujenga  mahusiano  mazuri  na waalimu wao kwa kuwa washauri wazuri kwa waalimu ili waweze kutumia vizuri fursa zilizopo katika Mkoa wa Katavi ili ziwasaidie kujiimarisha kiuchumi
Alisema kikao hicho cha kazi  ni vema  kiwasaidie pia  kuzingatia  wajibu wao  wa kuwajengea  waalimu uwezo  na moyo mzuri wa kufanya kazi  kwa kuwaboreshea  mazingira yao ya kufanyia kazi  ili wawe na moyo  katika ufundishaji  ambao utapelekea  wanafunzi  kufaulu vizuri katika mitihani yao
Alieleza ni vizuri viongozi wakajipima katika ngazi zao   za mamlaka ili waweze kujiuliza ni kwanini viongozi wengine  wanafanya vizuri  ili nawao  wajifunze kupitia kwao  endapo watafanya hivyo  maendeleo  ya elimu katika Mkoa wa Katavi  yataimarika
Aidha aliwataka viongozi wa elimu wa Mkoa huu kuzisimamia kwa ukaribu Halmashauri zao  ili mkoa wa Katavi upate  matokeo mazuri zaidi ya ufaulu  wa mitihani   matokeo ya mtihani  wa darasa la saba  mwaka 2013 Mkoa wa Katavi  ulikuwa wa 13 kati ya mikoa  25  ni vema sasa mkoa ukajipanga vizuri ili uweze kushika nafasi ya juu zaidi
Pia alizitaka Halmashauri  kuhakiisha zinasimamia  kikamilifu  ujenzi wa  maabara  katika  shule zao  za sekondari kama ambavyo alivyokuwa amewaagiza ili  zianze kutumiwa na wanafunzi  kwani maabara hizo zilipaswa kukamilika Desemba mwaka jana  2013
Hivyo atahakisha  anapita kukagua   kwenye Halmashauri zote  ili kuona hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa majengo ya maabara kwenye Sekondari zote na sehemu atakapo kuta  ujenzi hauja fanyika  hata sita kuchukua hatua  stahiki  kwa wale walioshindwa kutekeleza kwani agizo hilo la ujenzi wa maabara ni la Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa