Thursday, December 19, 2013

MAJAMBAZI WAVAMIA KIJIJI NA KUPORA KWA KUTUMIA BUNDUKI‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi

Watu watano wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi  wakiwa na silaha  bunduki  iliyotengenezwa  kienyeji  ambayo inatumia risasi  za SMG  wamevamia kijiji cha Katisunga  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele Mkoani hapa  na kuwapola wananchi  zaidi ya shilingi laki saba na  simu za aina mbalimbali

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina  Dhahiri Kidavashari  tukio hilo lilitokea  hapo Desemba 15  majira ya saa mbili na nusu  usiku katika kijiji hicho cha Katisunga

Alisema siku hiyo ya tukio majambazi hao ambao walikuwa na Bunduki  iliyokuwa imetengenezwa kienyeji  ambayo ilikuwa ikitumia risasi   za SMG walifika  kijijini hapo na kuwavamia wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wafanyabiashara  wa vibanda vya kuuza vocha  na kutowa huduma ya M—pesa  baada ya kuwatisha kwa kufyatua risasi hewani

Aliwataja waliopolwa na majambazi hao kuwa ni  Richald  Thomas  aliyepolwa pesa tasilimu Tsh 320, 000  na simu tatu za wateja ambao walikuwa wamezipeleka kuchaji  Samwel  Tito  alipolwa  pesa tasilimu Tsh  320,000 na simu  za aina mbalimbali za wateja wake

Kamanda Kidavashari  aliwataja watu wengine waliopolwa kuwa ni  Joyce  Msomba  aliyepolwa pesa  Tsh 100,000 na simu  moja  ya kichina  na Mohamed  Mrisho  aliyepolwa pesa Tsh 20,000 na kufanya jumla ya pesa zilizopolwa katika tukio hilo kuwa ni Tsh 740,000 NA Simu zenye thamani ya Tsh 450,000

Alisema  mtu mmoja  aitwaye  Justine  Mkolwa 21  mkazi wa mtaa wa Makanyagio Wilaya ya Mpanda  dereva  wa gari  aina ya Totota  Hiluxe lenye namba za usajiri  T800 ARN amekamatwa kuhusiana  na tukio hilo
Aidha alieleza  kuwa  upelelezi wa tukio hilo  bado unaendelea ilikuwabaini wale wote waliohusika na tukio ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

No comments:

Post a Comment