Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Masunga Nnigo(38) Mkazi wa Kijiji
cha Tumaini Kata ya Itenka Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi amejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na watu watatu kutokana
na mgogoro wa kugombea shamba la Hekta tatu
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea
hapo Desemba 15 mwaka huu majira ya saa moja na nusu asubuhi huko
katika kijiji cha Tumaini
Alisema siku hiyo ya
tukio Masunga alikuwa shambani kwake akilima mazao katika shamba
hilo ndipo walipotokea watu watatu wakiwa na panga na kisha walianza
kumkata kata kwenye mkono wa kushoto na kwenye nyonga upande wa
kushoto huku wakimtaka asirudie tena kulima kwenye shamba hilo kwani
walidai sio mali yake
Masunga baada ya kuona anaendelea kushambuliwa na watu hao alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zake
Alisema
majirani baada ya kusikia mayowe ya Masunga walifika katika eneo hilo
na kukuta watuhumiwa hao wakiwa wamesha tokomea huku Masunga akiwa
anavuja damu kwenye mkono wake wa kushoto kutokana na kukatwa katwa
vibaya sehemu hiyo ya mkono
Majeruhi amelazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako anaendelea kupatiwa matibabu huku
hari yake ikiwa bado sio nzuri kutokana na majeraha aliyoyapata
Kamanda Kidavashari alieleza watu wawili wanashikiliwa
na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo ambao ni Ndasa Wandasa 54
na Mgudi Ndasa 27 wakazi wa kijiji hicho cha Tumaini ambao wamekuwa na
ugomvi wa kugombea shamba na Masunga
Upelelezi wa tukio hili
unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada
ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika ili waweze kujibu mashitaka
yatakayo kuwa yamewakabili
No comments:
Post a Comment