N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Beritine Batazal 42 Mkazi wa Kijiji cha Mwese Wilaya ya Mpanda amekufa baada ya basi dogo alilokuwa akisafiria kupinduka baada ya kuacha njia na kusababisha watu wengine 19 kupata majeruhi na kulazwa Hospital
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahiri Kidavashari ajari hiyo ilihusisha basi dogo aina ya Hino lenye namba za usajiri T 894 APW lililokuwa likiendeshwa na mmiiliki wa gari hilo Dickson Kinyonto ambae alitoroka baada ya kutokea tukio
Kidavashari alieleza ajali hiyo ilitokea hapo Desemba 16 majira ya saa sita na nusu mchana katika eneo la Ilembo umbali wa kilimeta tatu kutoka Mpanda mjini barabara ya Mpanda ya kwenda Sumbawanga Mkoa wa Rukwa
Alisema gari hilo ambalolilikuwa litikokea Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele likielekea Mpanda mjini lilipata ajali hiyo baada ya taili lambele la upande wa kushoto kupasuka na ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Beritine na majeruhi 19 ambao wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda na watatu kati yao hari zao sio nzuri
Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi hao kuwa ni Charles Sokoni 25 mkazi wa mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda ,George Sengeka 48 mkazi wa Mpimbwe, January Damiano 38 mkazi wa mtaa wa Kasimba Ezekiel Benjamin 44 mkazi wa Kashaulili Mpuluku Magobo mkazi wa Ikingwa Saimoni Bala 25 Mkazi wa kata ya Kibaoni
Majeruhi wengine ni Paul Clement 28 mkazi wa kijiji cha Tinde Lyoba Mengo 36 mkazi wa Majimoto E 3170 CPL Albano polisi wa kituo cha Kibaoni Selemani Njala 62 mkazi wa kijiji cha Sosayati Magret Cosmas 29 Usinge Justine Michael 17 Bariadi Shinyanga , Cristina Gabriel 60 Stalike Mlele , na Kabura Sahani Majimoto Mpimbwe
Kidavashari alisema majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na mwili wa marehemu Beritine wamekabidhiwa ndugu zake kwa ajali ya mazishi yatakayo fanyika kesho kijijini kwao mwese
Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtumiwa dereva wa gari hilo Dickson Kinyonto ambae alitoroka baada ya Tukio ili aweze kufukishwa mahakamani kujibu tuhuma za kusababisha ajali
No comments:
Post a Comment