Home » » INASIKITISHA SANA : AUA MTOTO WA KAMBO KWA VIBOKO‏

INASIKITISHA SANA : AUA MTOTO WA KAMBO KWA VIBOKO‏

Na   walter mguluchuma
Mpanda
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili  mkazi wa Kijiji cha Majalila wilaya ya Mpanda ameuwawa kwa kupigwa na fimbo kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake  na baba yake  wakambo  aitwaye  Hamisi Mohamed.

Tukio hilo lilitokea hapo juzi majira  ya usiku wakati moto huyo  alipokuwa amelala kitandani na wazazi wake 
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari alisema marehemu huyo alikufa baada ya baba yake wa kambo kukasilishwa na kitendo cha mtoto huyo kulia wakati akiwa amelala kitendo ambacho aliona kinamnyima usingizi.

Alisema kitendo hicho cha  marehemu kulia kilimfanya baba huyo wa kambo kimkasilishe na ndipo alipoanza kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake huku mama wa motto akimsihi baba huyo wa kambo aache kumpiga mtoto huyo.

Alieleza baada ya kuona hari ya motto huyo imekuwa mbaya baba huyo wa kambo alimuaga mkewe kuwa anakwenda dukani kumnunulia dawa  za maumivu.

Baada ya baba huyo wa kambo kwenda dukani motto huyo alifarikibaada ya muda mfupi toka baba yake huyo wa kambo alivyokuwa amekwenda dukani ambapo alitokomea kusiko julikana.

Kamanda Kidavashari alisema uchunguzi wa awali  wa baba wa kambo  kumuuwa mtoto huyo ni chuki baina ya mama wa mtoto huyo aitwaye Diana Philipo  na mume wake  ambae akutaka marehemu aishi nyumbani kwake.

Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliakikamatwa afikishwe kwenye vyombo vya sharia



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa