Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halimashauri ya
Mji wa Mpanda inatajia kupata shilingi
Bilioni kumi na mbili kwa ajiri ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali za
Halmashauri hiyo katika Mjiwa wa Mpanda
Hayo yalisemwa
hapo juzi na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga
kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halimashauri hiyo kilichofanyika katika
ukumbi wa chuo kikuu huria cha Mkoa wa Katavi
Lukanga alieleza
kuwa fedha hizo shilingi Bilooni kumi na mbili
zinatolewa na Serikari kwa mkopo wa kutoka Benki ya Dunia
Alitaja miundo
mbinu zitakazo tengenezwa kuwa ni ujenzi
wa soko kubwa la kisasa katika eneo la soko la zamani na ujenzi wa sitendi
ya mabasi katika eneo la Ilembo
Aliitaja miundo
mbinu mingine kuwa ni ujenzi wa barabara
zenye urefu wa kilometa saba kwa kiwango cha lami katika barabara za
mjini pamoja na ujenzi wa mitalo katika mitaa mbalimbali ya mji huu
Alieleza kuwa
wataalamu mbambali wanatarajiwa kufika
hivi kalibuni kwa ajili ya kuangalia maeneo hayo kwa ajiri ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa miundo mbinu hiyo
Pia aliesema
Halimashauri imepanga kujenga sehemu ya
kuegesha magari makubwa katika maeneo ya Misunkumilo kwa ajiri ya magari yanayo
toka Mkoa wa Kigoma na Ilembo kwa ajiri ya magari yanayotoka Sumbawanga na
Tabora
Alifafanua kuwa
Halimashauri imeamua kujenga maeneo ya kuengesha magari ya mizigo kufuatia
magari hayo kuwa yamekuwa yakifanya
uharibifu wa barabara za lami zilizopo mjini hapa na kutokana na kuwa na uzito mkubwa na yamekuwa
yakipaki katika maeneo yasiyo lasimi
kama vile kwenye nyumba za kulala wageni na matokeo yake Halimashauri imekuwa
ikikosa mapato
0 comments:
Post a Comment