Na Walter Mguluchuma-Blogs za Mikoa
Nkasi.
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka 60 jela wakazi wawili wa wilaya hiyo baada ya kupatikana na makosa mawili tofauti ya kulawiti na kubaka.
Adhabu ya kwanza imemkuta Kalutwa Sumbizi mkazi wa kijiji cha Utinta kata ya Kabwe ambaye amepatikana na hatia ya kumlawiti mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka (7).
Katika kesi hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Sumbawanga Manase Goroba, aliyeridhishwa na maelezo ya upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi Mratibu msaidizi Hamimu Gwelo uliodai kuwa kijana huyo alitenda kosa hilo kwenye moja ya pori kijijini hapo.
Gwelo alisema kuwa siku ya tukio Sumbizi alimkuta mtoto huyo akiwa anachunga mbuzi kwenye pori hilo ambapo alimwita na kumtaka amfuate alikokuwa akielekea ili akampatie nyama ya sungura.
Baada ya mtoto huyo kumfuata na kufika mbali zaidi Sumbizi alimlazimisha mtoto huyo kuvua nguo na kumfanyia unyama huo kabla ya kukutwa na mtu mmoja ambaye alipomuona alitimua mbio.
Jitihada za Sumbizi kutoroka ziligonga mwamba baada ya mtu huyo kupiga kelele za kuomba msaada na baadaye kufanikiwa kumkamata Sumbizi akiwa amejificha kando ya bwawa moja kijijini hapo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Goroba alisema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na hakiwezi kuvumiliwa hivyo anatoa adhabu hiyo kama funndisho kwa watu wengine wa aina hiyo.
Katika kesi ya pili hakimu huyo pia amemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela Peter Mwananjela (26)mkazi wa kijiji cha Kakoma kata ya Kirando kwa kosa la kumbaka mwanamke mmoja kijiji hapo.
Mwendesha mashata Hamimu Gwelo aliiambia mahakama hiyo kuwa Mwanajela alimbaka mwanamke huyo ambaye alikuwa mfanyakazi wa moja ya baa kijijini hapo akiwa amelala chumbani kwake.
Gwelo alisema kuwa Mwanajela alifanikiwa kuingia kwenye chumba hicho kwa kupitia dirishana na kufanya kitendo hicho baada ya kumkaba mwanamke huyo na kumziba mdomo kabla kupiga kelele za kuomba msaada na kukimbizwa na kundi la watu hatimaye kukamatwa.
www.blogszamikoa.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment