NaWalter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Gemela Lubinga amewalaumu watumishi wa Idara ya Maliasili na Mazingira wa Wilaya hiyo kwa kutokuwa waaminifu katika majukumu yao ya kazi
Kauli hii aliitowa hapo juzi mbele ya waandishi wa habari wakati alipokuwa akizungumza nao ofisini kwake akiwaelezea namna ya shughuli mbambali za utekelezaji wa maendeleo zilizo fanyika katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita na kutekelezwa wilayani Mlele.
Alisema idara ya Maliaslili inaonekana kutokuwa na watumishi waanifu na hari hiyo imekuwa ndio chanzo cha watu kuvuna mbao kwenye maeneo yasiyo sitahili na kusababisha uharibifu wa mazigira
Alieleza kuwa yeye Mkuu wa wilaya mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya msako kwenye maeneo ya Game Reserve ya Mlele na kufanikiwa kukamata watu wakiwa wanachana mbao mwenye maeneo hayo na aliweza kukamata mbao 3000 za aina ya mninga
Alifafanua kuwa Serikali imekuwa ikitoa pesa kwa watumishi wa idara ya Maliasi kwa ajiri kulipa wakafanye kazi za kuwasaka watu wanao vamia maeneo ya misitu lakini kazi hiyo wamekuwa hawaifanyi ipasavyo
Kama mimi kwa muda wa siku moja nimeweza kukamata watu na mbao hizo wao huwa wako wapi.
Matokeo yake serikali imekuwa ikiingia gharama kubwa ya pesa na matumizi ya gari kwa ajili ya watumishi wa maliasili wanapokwenda kufanya msako lakini inaonekana kazi hiyo haifanyiki kwa ufanisi alisema Lubinga
Alisema kutokana na watumishi wa wa idara hiyo kutokuwa waaminifu kuna weza kukaisababishia wilaya hiyo na Nchi kwa ujumla hasara itokanayo na uharibifu wa mazigira
Alieleza kuwa maeneo mingi ya hifadhi za misitu katika wilaya ya Mlele yamevamiwa na wachana mbao ambao baada ya kuzichana zimekuwa zikisafirishwa kinyemelana wafanya biashara hiyo kuyoka mikoa yaMwanza Moshi Tabora na Dares salam
0 comments:
Post a Comment