Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Umoja wa wazee wa mkoa wa Katavi wamefanya mkutano wa kushauliana na kubolesha masilahi ya wazee pamoja na kuanzisha mfuko wao ili waweze kuwa na dhamana ya kupata mikopo kwenye benki mbalimbali hapa nchini.
Mkutano huo ulifanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Super City uliopo mjini Mpanda ambao uriwashilikisha pia viongozi wa halmashauri za mji na wilaya pamoja na tasisi za fedha.
Wazee hao kwa pamoja waliiomba serikari kuwaingiza wazee katika agenda ya mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za kijiji hadi taifa.
Pia walijadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee hapa nchini ambazo walizitaja kuwa ni wazee kutokuwa na wawakilishi katika vikao vya maendeleo na maamuzi
Pia walidai wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na Daktarii aliye bobea kwenye utaalamu wa kuwatibu wazee pindi wanapo kuwa wamepatwa na maradhi mbalimbali.
Walitaja pia walilalamikia sera za mabenki hapa nchini za kutowaruhusu wazee kuwakopesha mikopo ambayo ingeweza kuwasaidia kujikimu kewnye maisha yao.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Mpanda Selemani Mbazi aliwaeleza wazee hao wakati akiwasilisha maada yake kuwa utaratibu uliopo wa mabenki hauna utaratibu wa kuwakopesha wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 63
Mbazi aliwashauri wazee hao kuweka utaratibu wa kuunda vikundi ili waweze kupata mikopo kwani watakuwa wameweza kutiza mashariti ya kupewa mikopo.
Kwa upande wake katibu mkuu wa mtandao wa mashirika ya wazee tanzania Top Wilison Karuwesa alisema kwenye mkutano huo kuwa idadi ya wazee hapa nchini kwa sasa imefikia wazee milioni 2 na ifikapo mwaka 2050 watakuwa wamefika asilimia 10 ya wantanzania wote hapa nchini
Alisema pamoja na wazee kubeba mizigo mizito bado umuhimu wao hauja tambuliwa kwenye jamii na serikarini kwa ujumla.
Miongoni mwa mizigo wanayo ibeba wazee ni kutunza yatima ambapo asilimia 70 wanatunzwa na wazee na waathirika asilimia 80 wana tunwa na wazee pia alisema Karuwesa
0 comments:
Post a Comment