na Walter Mguluchuma
Mpanda
Akina mama wajawazito wa Mkoa wa Katavi wametakiwa kuachana na tabia ya kuchelewa kwenda hospitalini na kwenye vituo vya afya kupima afya pindi wanapo kuwa wamepata ujauzito ili kuepuka vifo vya mama na mtoto.
ushauri huo ulitolewa hapo juzi na mbunge wa viti maalumu mkoa wa katavi Dr Pudensiana kikwembe alipo kuwa akizungumza na akina mama wajawazito kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alipo kuwa akiwafariji wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya krismasi.
Dr Kikwembe (CCM) mbali ya kuwafariji wakinana wajawazito pia aliwapatia vitenge kwa akina mama wote 45 walio kuwa wamelazwa ndani ya wodi hiyo pia alitowa chakula kwa wagonjwa wote na vinywaji baridi katika wodi zote sita za hospitali hiyo ya wilaya ya Mpanda.
Mbunge huyo alisema ni vizuri watu wakapatiwa elimu ya afya ili kuepukana na tatizo sungu lililopo Mkoani Katavi la kuwachelewesha wagonjwa walio wengi wanao kuwa wagonjwa wanapelekwa hospitalini wakiwa wameshoka kutokana na kutopelekwa mapema Hospitalini.
Alifafanua kuwa madakitari wamekuwa wakipewa lawama ambazo sio zao ili kuokoa uhai watu wawe na tabia ya kutibiwa mapema na sio kukimbilia kwanza kwa waganga wa kienyeji ambao sio wataalumu wa kuweza kutambua magonjwa mbambali.
Dr Kikwembe aliwashauri akinana mama wajawazito na wazazi kwa kufuata mashariti ya afya kwa kutumia vyandarua ili kuepukana na vifo vinavyo sababishwa na ugonjwa wa maralia na pia kumuunga mkono mama Salima Kikwete kwenye jihihada zake za kupambana na ugonjwa wa maralia.
Alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipewa msaada wa vya ndarua na wao wamukuwa wakivitumia kwa matumizi mengine ya kuvulia samaki na kufungia kuku hivyo amewataka waachane na tabia hiyo.
Pia aliwashauri wakinamama wajawazito wawashirikishe waume zao pindi wanapo kuwa wanaenda cliniki ili na wao wanaume waweze kuwa wakijua maendeleo ya afya zao tofauti na ilivyo sasa ambavyo inaonekana swala la cliniki linamhusu mama mjamzito peke yake.
Dr Kikwembe aliwaomba madakitari na wauguzi waendelee na moyo wa kufanya kazi licha ya upungufu uliopo wa watumishi wa idara ya afya kwani serikali inalitambua hilo na ndio maana ina mpango wa kuongeza vyuo yva madakitari na wauguzi
Kwa upande wake muuguzi mkuu wa hospitali hiyo Evelina Wampembe alimshukuru Mbunge huyo wa viti maalumu na amewaomba viongozi wengine waige mfano wake
Pia wampembe alisema kuwa hospitali hiyo inakabilwa na changamoto mbalimbali ikiewepo ya upungufu wa watumishi wa affa ambapo waliopo ni 50 wakati mahitaji ni watumishi 150
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni miundo mbinu mibovu ya vyoo vya nje ambavyo ni vyakizamani vya matundu ya chuo ambapo husababisha baadhi ya kuna mama wanapo jifungua kutupia mtoto kwa makusudi.
Muuguzi huyo wa Hospitali alieleza kuwa katika skukuu ya krismasi jumla ya watoto 13 walizaliwa katika wodi hiyo ambapo watoto kumi walikuwa ni wakiume na tatu walikuwa ni wakike.
0 comments:
Post a Comment