Home » » KAMATI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KATAVI (KAREFA) WASIMAMISHIWA UCHAGUZI‏

KAMATI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KATAVI (KAREFA) WASIMAMISHIWA UCHAGUZI‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu cha mkoa mpya wa Katavi (KAREFA)  ambao ulikuwa ufanyike leo mjini mpanda umesimamishwa na kamati ya uchaguzi ya TFF Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo mkoa wa Katvi Dezidelius Magezi alisema kuwa amepokea barua hapo jana ikimwagiza kutofanya uchaguzi huo.
Alieleza kuwa barua hiyo ya kusimamisha uchaguzi imetokana nakamati ya uchaguzi ya TFF Taifa kutaka kuridhika na baadhi ya sifa za wagombea.
Kufuatia hari hiyo wameiagiza kamati ya uchaguzi mkoa wa Katavi kutuma vyeti halisi vya wagombea watano kwenye kamati ya uchaguzi ya TFF Taifa na wagombea hao wanatakiwa Novemba 12 wawe wamekabidhi vyeti hivyo kwenye kamati ya uchaguzi ya mkoa wa Katavi
Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni Mwenyekit ambapo wagomgbea walikuwa wawili, Katibu mkuu wagombea wawili na Makamo Mwenyekiti alikuwa mgombea mmoja.
Nafasi nyingine zilizokuwa zikigombewa ni nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Taifa iliyokuwa na wagombea wawili na mjumbe wa kuwakilisha vilabu mgombea alikuwa mmoja.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa