Home » » MAHINDI YAKWAMA KUSAFIRISHWA KATIKA KITUO SHA RELI MPANDA KUTOKANA NA UKOSEFU WA MABEHEWA

MAHINDI YAKWAMA KUSAFIRISHWA KATIKA KITUO SHA RELI MPANDA KUTOKANA NA UKOSEFU WA MABEHEWA

Shehena za mahindi zikiwa zimerundikana katika kituo cha shirika la reli (TRL) kituo cha Mpanda baada kushindwa kusafirishwa kwenda Mikoa ya kanda ya ziwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.


Alhamisi ya wiki iliyopita wafanya biashara wa mahindi wanaosafirisa mazao hayo waliamua kulala kwenye mataruma ya reli kuizuia treni ya mizigo iliyokuwa inakwenda kuchukua mahindi kwenye maghala ya akiba ya chakula cha Taifa yaliyopo karibu na kituo cha reli cha Mpanda.

Lengo la wafanya biashara kulala katika mataruma ya reli walikuwa wanalishinikiza shirika la reli liwasafirishie mazao yao wakihofia kuharibika kwa mvua za msimu wa kilimo zinazo tegemea kuanza kunyesha mwezi ujao.

Picha na Walter Mguluchuma

Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa