Na Water Mguluchuma
Mpanda- Katavi yetu Blog
Mwanamke mmoja mkazi wa kitongoji cha Rosiha kata ya Litapunga wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi ameuwawa akiwa nyumbani kwake kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasio julikana.
Diwani wa kata hiyo Godfrey Lusambo amemtaja aliye uwawa kuwa ni Mwajuma Joseph (60) mkazi wa kijiji cha Kambuzi kata ya Litapunga
Alisema tukio hilo lllltokea hapo Agosti 6, mwaka huu majira ya saa mbili na nusu nyumbani kwa marehemu aliko kuwa anaishi peke yake.
Alisema diwani huyo kuwa katika tukio hilo la kumkataka kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wa mwanamke huyo hakuna mali yoyote ambayo ilichukuliwa.
Hari hiyo ina onyesha kifo hicho kilitokana na imani za kishilikina alieleza kwa masikitiko makubwa diwani Lusambo.
Diwani huyo amewaommba wananchi wa eneo hilo kutowa ushirikiano kwa vyombo vya dola utakao saidia kukamatwa kwa watu hao.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo imekuwa na mauaji ya mara kwa mara ya vikongwe.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment