Friday, August 3, 2012

MENEJA KAMPUNI YA WACHINA MIAKA MINNE JELA KWA KUCHIMBA MADINI KWENYE HIFADHI.

Na Walter Mguluchuma, Mpanda – Katavi yetu
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya  ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu Mkurugenzi wa Kampuni ya Kichina ya REDORE yenye makao yake Makuu Mjini Dar es salaam ya uchimbaji wa madini kifungo cha miaka minne jela baada ya Kampuni kupatikana na hatia ya kuchimba Madini katika eneo la kuhifadhi wavyama na Misitu.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya China Bloana Chaoxan 2hou (42) aliweza kulipa faini ya shilingi 1,850,000/= kufuatia mahakama hiyo kutoa adhabu mbili kwa pamoja za kifungo au faini ambapo aliweza kulipa kulipa faini na kuachiwa huru kwa masharti ya kutotenda kosa lolote lile tena ndani ya kipindi cha  Mwaka Mmoja.

Awali katika kesi hiyo mwanasheria wa serikali wa Moa wa Rukwa  Prospa Rweyongira aliieleza Mahakama mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi Richald Kasele kuwa Kampuni hiyo iliingia kuchimba madini katika hifadhi ya Wanyama ya Rwafi bila kuwa na kibali.

Mwanasheria huyo wa Serikali alimsomea Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Kichina jumla ya mashitaka sita hapo jana na raia huyo wa China na alikili makosa hayo.

Mashitaka hayo sita aliyosomewa ni kuingia ndani ya Hifadhi, bila kibali kufanya uharibifu wa mazingira, kuchimba madini ya Hifadhi ya Wanyama na misitu.

Mashitaka mengine ni kujenga na kuchimba madini ya hifadhi kuendesha migodi ndani ya hifadhi bila kuwa na mikataba na shirika la sita lilikuwa ni kuendesha migomdi eneo ambalo limekatazwa kisheria za madini na wanyama.

CHAOXAN baada  ya kusomewa mashtaka na mwanasheria wa Serikali alikiri kutenda makosa hayo kwa kile alichokieleza hakufahamu kama eneo hilo aliruhusiwi kuchimba madini.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa hata yeye Kampuni yake iliuziwa kibali hicho hivyo walio wauzia ndio walio watapeli kwa kuwapatia kibali bandia cha kuchimbia madini ambayo hairuhusiwi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Kasele baada ya mshitakiwa kukiri makosa hayo sita aliieleza Mahakama  kuwa Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kama ifuatavyo kosa la kwanza Mahakama inamhukumu mshitakiwa kufungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi 200,000/= na kosa la pili jela Miaka Minne au faini shilingi 250,000/=.

Shitaka la tatu  jela miezi sita au faini shilingi 300,000/= shitaka la Nne jela miezi sita au faini shilingi 300,000/= na shitaka la tano walimuachia kwa shariti la kutotenda kosa lolote kwa kipindi cha  mwaka mmoja  na kosa la sita ilikuwa kulipa shilingi 300,000/= au kwenda jela miezi sita ambapo mshitakiwa aliweza kulipa faini hizo na kuachiwa huru.

Hakimu Mkazi Kasele pia aliingiza Kampuni hiyo kubomoa majengo yote iliyokuwa imejenga na kufukia mashimo yote waliyo kuwa wamechima kwenye eneo hilo la hifadhi.
Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment