Na Walter mguluchuma
Mpanda-Katavi yetu Blog
Serikali ya wilaya ya mlele mkoa wa katavi imepanga kumaliza tatizo linalowakabili baadhi ya wakazi wa kata ya majimoto wilayani hapa la upungufu wa maji
Mkuu wa wilaya ya mlele Ngemela Lubinga alisema serikali imepanga kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa maji katika kata hiyo.
Alisema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na benku ya dunia wameanza mpango wa kuwafikishia maji wananchi wa kata hiyo ambayo yatatengwa kutokea katika milima ya Lyambalyamfipa.
Hivyo aliwaomba wananchi wa kata hiyo wawe na subira kidogo kwani serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ina kwenda hatua wa hatua.
Alieleza ndio maana serikali ya wilaya ya mlele ilitoa madawati kwa shule ya kata hivi karibuni ambayo yanawatosha kutumia watoto mia tatu hivyo inaonyesha ni jinsi gani matatizo yenu yanavyo shughulikiwa.
Sio kweli kama baadhi ya watu wanao wadanganya kuwa serikali haiwajali wananchi wa kata ya majimoto alisema Lubinga
Pia alieleza kutokana na shule yao ya msingi ya kata yao majimoto kuwa na wanafunzi wengi kupita kiasi halmashauri ya wilaya hiyo imepanga kujenga shule nyingine katani hapo.
Alisema shule hiyo itakapokamilika kwa kushirikiana na nguvu ya wananchi itasaidia kupunguzza msongamano wa wanafunzi uliopo sasa
No comments:
Post a Comment