Saturday, August 4, 2012

DC MPANDA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA KUUNGANISHA BADALA YA KUTENGANISHA JAMII

Na Walter Mguluchuma, Mpanda-katavi yetu

Waandishi wa habari wametakiwa kutumia taaluma yao vizuri kwa kuandika habari zinazo unganisha jamii sio za kuwatenganisha.

Wito huu umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya mpanda Paza Mwamlima wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maswala ya maendeleo ya Wilaya ya hiyo.

Alisema wapo baadhi ya waandishi wamekuwa wakitumia vibaya taaluma hiyo kwa kuandika habari za kuitenganisha jamii badala ya kuwaunganisha.

“Watanzania wengi wanaamini kile kinacho andikwa na kutolewa na vyombo vya habari ndiyo sahihi hivyo waandishi msiandike habari za kupotosha jamii” alisema Mwamlima.

Aliwata waandishi wa habari kujiepusha na baadhi ya watu ambao wanataka kuitumia vibaya demokrasia iliyopo.

Aidha Mwamlima amewataka wananchi wa Wilaya ya Mpanda kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye kamati ya tume ya kupokea maoni ya kurekebisha katiba itakayoanza kufanya mikutano Wilaya Mpanda mwezi huu.

Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment