Saturday, July 28, 2012

TAARIFA YA KUSIKITISHA: WANNE WAUWAWA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI LIKIWEMO LA WANANDOA WAWILI KUKATWA KATWA KWA MAPANGA


Mpanda- Katavi Yetu Blog
Na Walter Mguluchuma
Watu wanne wameuwawa katika matukio mawili tofauti mkoani katavi likiwemo la kufa katika kijiji cha matandalani wilayani mlele.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari alisema katika tukio la kwanza lililo tokea julai 23 mwaka huu ambapo costantino Mwanjela (59) na mkewe Evodia Kidoma (36) wakazi wa kijiji cha matandalani wilayani mlele waliuawa na watu wasio julikana na wakati wakiwa wamelala kitandani.
Alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi uliobaini kabla ya tukio hili kulikuwapo mgogoro wa shamba la marehemu na George Mchina ambaye alidaiwa kulishia mifugo yake ya ng’ombe kwenye shamaba la marehemu.
Kidavashari alisema kufuatia mazao hayo ya marehemu kuliwa na mifugo aliamua kwenda kumshitaki George Mchina kwa balozi aitwaye Mgombola Budito na katika malalamiko hayo walikubaliana kuwa marehemu alipwe fidia ya shilingi 17000= hapo tarehe 24/7/2012 kama fidia ya uharibifu wa mazao yake.
Kamanda Kidavashari alisema ilipofika siku ya tarehe 23/7 mwaka huu marehemu na mke wake waliuwawa usiku wakiwa wamelala kitandani baada ya kukatwa katwa na mapanga.
Kufuatia tukio hilo polisi walimkamata mdaiwa, balozi na mkewe aitwaye Tatu Cherles ambaye ni mjomba wa mdaiwa kwa ajili ya mahojiano.
Alieleza polisi waliweza kufuatilia tukio hilo na ndipo walipo weza kufanikiwa kukuta panga ndani ya nyumba ya George Mchina huku likiwa na damu zinazokisiwa kuwa ni za marehemu hao wawili.
Baada ya kukamata panga hilo miili ya marehemu hao wawili wanandoa ilichukuliwa damu zao pamoja na damu za George kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na damu iliyopo kwenye panga hilo.
Tukio la pili lilitokea Juali 24 mwaka huu huko katika kijiji cha Mwamkulu wilayani mpanda ambapo watu wawili wameuwawa na wananchi kwa tuhuma za wizi wa mpunga gunia moja mali ya Mhoja Maziku.
Kamanda Kidavashari amewataja waliouwawa kwenye tukio hilo kuwa ni Datus Kaegele (35) wa Senjajohn kijiji cha mwamkulu wilayani mpanda na marehemu wa pili hakuweza kutambulika jina ambaye ni mkazi wa uwanja wa ndege mjini mpanda.
Baada ya mpunga huo kuibiwa wananchi walianza kufuatilia na ndipo walipokuta mpunga huo ulioibiwa ukiwa umefichwa porini hari ambayo iliwafanya wananchi hao kuamua kujificha porini ili kuona mtu ambaye atakuja kuuchukua mpunga huo.
Kamanda Kidavashari alisema ndipo walipo waona marehemu hao wawili wakiwa na baiskeli na mifuko mitupu ya sandarusi na kuanza kuchukua mpunga huo.
Wananchi hao  waliokuwa na hasira waliweza kuwapiga na hatimaye kuwauwa na kuwachoma moto pamoja na mali hizo
Katika tukio hilo watu wanne akiwemo mwenye mpunga huo ulioibiwa aliyetajwa kwa jina la Mhoja Maziku na wenzake watatu ambao no Michael Rehani (66) George Joseph Mbesambili (30) ambaye ni mtendaji wa kijij cha Mwamkulu na Lauriano Marimi Ngaru ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamkulu wanashikiliwa na polisi kuhusiana na mauaji ya watu hao wawili waliouwawa na kuchomwa moto.
Kamanda wa polisi mkoa wa katavi ametoa rai kwa wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwa kuwauwa watuhumia na badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake
Pia amewaomba wananchi wa mkoa wa katavi kuhakikisha wageni wote wanaoingia kwenye maeneo ya vijiji na vitongoji taarifa zao zipelekwe kwa viongozi wa ngazi husika kwani matukio mengi ya watu wana

No comments:

Post a Comment