Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi yetu blog
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imetoa shilingi milioni kumi kwa hospitali ya wilaya yam panda mkoa wa katavi kwa ajiri ya kununulia dawa.
Fedha hizo zimetolewa kufuatia hospitali hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa dawa kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa.
Mganga mkuu wa mkoa wa katavi Dr. Yhaya Hussein alieleza kuwa tayari wizara ya afya na ustawi wa jamii imeisha towa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajiri ya kununulia dawa za hospitali hiyo.
Dr. Yaahaya ameeleza kuwa upungufu huo wa dawa ulitokana na wizara ya afya na ustawi wa jamii kuchelewa kuipatia hospitali hiyo yawilaya yam panda pesa kufuatia kusubilia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.
Alisema mpaka mwishoni mwa wiki hii dawa hizo zitakuwa zimefika wilaya yam panda tayari kwa matumizi ya wagonjwa mbalimbali.
Wagonjwa mbalimbali waliolazwa katika hospitali hiyo inawalazimu kwenda kununua dawa katika maduka yaliyopo mitaani na wamekuwa wakipata shida hasa majira ya usiku
Mbali ya ukosefu wa dawa za binadamu vilevile kuna ukosefu wa sindano (sirinji) ambazo pia inawalazimu kuzifuata kwenye maduka ya mitaani
Wakazi wa wilaya ya mpanda hutumia hospitali hiyo ya wilaya kama ndio hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi kutokana na kutokuwa na hospitali nyingine vilivyopo ni vituo vya afya ambavyo vipo katika tarafa za mkoa huo.
No comments:
Post a Comment