Monday, July 30, 2012

AJALI YA FUSSO YAUA WAWILI NA KUJERUHI 15.


Na Walter Mguluchuma, Katavi
WATU wawili wamekufa na wengine kumi na tano kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Mpanda kufuatia Roli walilokuwa wakisafiria kupinduka Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi majira ya saa 9:00 Mchana katika Barabara ya Mpanda kwenda Tabora katika eneo la Mlima Kanono.
Aliwataja watu wawili walio kufa kuwa ni Mbungwe Kalemani (34) mkazi wa Mwamkuru Mpanda na Kaswendebaza Makude (28) Mkazi wa Salani Mkoani Shinyanga ambaye alikuwa ni utingo wa gari hiyo.
Alisema kuwa miili ya marehemu hao wawili bado imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika Hospitali ya Mpanda na hali za majeruhi waliolazwa zinaendelea vizuri.
Kidavashari amewataja waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitari ya Wilaya ya Mpanda kuwa ni pamoja na Gedfrey Jonas (29) Mkazi wa Mwanza aliyepata maumivu ya kifua, Lucas Charles (30) Mkazi wa Kabage Mpanda na Joseph mafulaya (31) Mkazi wa Isege Nzega.
Wengine ni Ally Shabani (20) Mkazi wa Nzega Tabora, Andrea Deus (25), Ruge Mchele (45), Kizimani Ruge (2) wakazi wa Mkoa wa Shinyanga, Masumbuko Amosi (28) Mkazi wa Sikonge Tabora, Saida Mashauri (32) Mkazi wa Sikonge Tabora na Marco Misayo (30) Mkazi wa NzegaTabora.
Kamanda Kidavashari amewataja majeruhi wengine kuwa ni Efulazi Pascal (45) Mkazi wa Inyonga Mlele, Mwazu Makanio (33), mkazi wa Mwamkuru Mpanda na Grece Magembe (22) Mkazi wa Meatu Shinyanga.
Alitaja Gari hilo lililopata ajari ni aina ya Fuso mali ya MAHARAGE Mkazi wa Shinyanga, lenye namba za usajili T476 ARR ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dreva aliyetambulika kwa jina moja la Emmanuel ambaye hata hivyo alikimbia mara baada ya ajari hiyo kutokea.
Kidavashari alieleza kuwa Gari hilo lililokuwa limebeba gunia 90 za mpunga kutoka Mpanda kupeleka Kahama lilipinduka baada ya kuacha njia na kuelekea porini.
Kamanda Kidavashari ameto wito kwa madereva wa magari kufuata Sheria na kuheshimu Sheria za usalama Barabarani ili kuepusha ajali nchini.




No comments:

Post a Comment