Home » » JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NYAMA YA KIBOKO ZAIDI YA KILO 110.

JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NYAMA YA KIBOKO ZAIDI YA KILO 110.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma .
   Katavi .
Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani  Katavi imemuhukumu   Omary  Maganga  45  Mkazi wa  Kijiji cha  Itenka  Rarafa ya  Nsimb0   Wilaya ya  Mpanda kutumikia  jela kifungo cha miaka    20  jela baada ya kupatikana na  hatia ya kukamatwa na  nyama ya Kiboko zaidi ya kilo 110  .
Hukumu  hiyo ilitolewa  hapo jana  na  Hakimu  Mkazi   mfawidhi wa  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada ya  Mahakama   kulidhika na  ushahidi uliotolewa  Mahakamani  hapo na   upande wa  mashitaka uliokuwa ukiongozwa na  Mwanasheria wa  Serikali   Fraviani   Shio.
Awali  katika  kesi  hiyo       mwendesha  mashitaka  mwanasheria wa  Serikali   Fraviani  Shio   alidai   Mahakamani  hapo  kuwa     mshitakiwa  Omary  Maganga  alitenda  kosa  hilo  hapo   Oktoba 10 mwaka 2016 majira ya  saa  kumi  jioni.
 Alidai kuwa  siku  hiyo ya tukio  mshitakiwa  alikamatwa   akiwa   ndani  ya  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  huku   akiwa  na   nyama ya  kiboko  yenye  uzito wa kilo 118 yenye  thamani ya  Tshs 3,274,500.
Mwanasheria   huyo wa  Serikali    aliiambia   Mahakama  kuwa  mshitakiwa  huyo  alikamatwa  na   askari wa   Hifadhi ya  Taifa ya   Katavi  baada  ya kuwa  wamepata taarifa kutoka kwa raia  wema za kuwa   mshitakiwa amekuwa akifanya ujangili kwenye hifadhi ya Taifa na  ndipo walipoanza msako na kufanikiwa kumkamata  siku  hiyo akiwa ndani ya Hifadhi ya Katavi huku akiwa na nyama hiyo ya Kiboko.
Akisoma  hukumu  hiyo   Hakimu  Chiganga  alisema  kuwa  kutokana  na   ushahidi uliotolewa  Mahakamani  hapo  na  upande wa  mashitaka  ambao  ulikuwa  na  mashahidi watano na  na  mshitakiwa  hakuwa  na  shahidi yoyote alisema   Mahakama  pasipo   mashaka yoyote imemwona  mshitakiwa   akiwa  amepatikana  na   hatia  ya kifungo cha sheria   Namba  86 kifungu   kidogo cha  kwanza na cha pili  cha   sheria ya  wanyama  pori  Namba 5 ya  mwaka  2009.
 Hivyo   kabla ya  kusoma  hukumu  alitowa  nafasi kwa  mshitakiwa ya kuweza kujitetea na  kama   anayosababu yoyote ya  msingi ya kuweza kuishawishi  Mahakama  iweze kumpunguzia   adhabu.
Mshitakiwa  Maganga    katika  utetezi wake  aliiomba  Mahakama impunguzie  adhabu  kwa kwa  kile aichodai    hilo  lilikuwa ni kosa   lake  la  kwanza  katika  maisha yake  na  pia  anayofamilia   ambayo  inamtegemea ya  mke na watoto pamoja na wazazi wake .
 Utetezi huo ulipingwa vikali na  mwanasheria wa  Serikali  Fraviani  ambae  aliiomba  Mahakama  itowe   adhabu kali kwa  mshitakiwa ili   iwefundisho kwa watu wengine  wenye  tabia ya kuhujumu uchumi wa  nchi.
   Hakimu  Chiganga  Ntengwa  baada ya  kuzisikiliza  mbili  aliiambia  Mahakama  kuwa  mshitakiwa  Omary  Maganga  kutokana   na makosa yaliomtia  hatiani   Mahakama  imemuhukumu kutumikia  jela kifungo cha miaka 20 kuanzia  jana  na  kama  haja ridhika   na  adhabu hiyo  inayonafasi ya kukata rufaa kwenye  Mahakama ya juu zaidi .

  MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa