Home » » AFIKISHWA MAHAKAMANI AKIWA NA MAKOSA MANNE LIKIWEMO NA LA UHUJUMU UCHUMI

AFIKISHWA MAHAKAMANI AKIWA NA MAKOSA MANNE LIKIWEMO NA LA UHUJUMU UCHUMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na   Walter  Mguluchuma.
 Mlele  Katavi

MKAZI wa Sumbawanga mjini mkoa Rukwa , Raphael Kusa (18) amefikishwa  katika Mahakama  ya Wilaya ya Mlele  mkoani   Katavi akishtakiwa kwa makosa manne   ya uhujumu uchumi  ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali zenye thmani ya zaidi ya Sh milioni 3.0
Mshtakiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu  Mkazi   Tiotemus Swai wa  Mahakama ya   Wilaya ya  Mlele  Mkoani  Katavi ambapo hakutakiwa  kujibu lolote  kwa kuwa makosa  yote manne  yameagukia  kwenye makosa ya uhujumu uchumi ambapo  mahakama hiyo haina malaka ya kuisikiliza  ilisipokuwa Mahakama Kuu .
Kusa anashitakiwa kwa makosa ya kukutwa na  bunduki aina  ya gobori , vilipuzi vyenye nuzito wa gramu 200 na risasi 21 za gobori bila kuwa na kibali halali ambapo ni kinyume  na Sheria ya  uthibiti wa silaha na risasi kifungu cha sheria namba 20(1) (2)  ikisomwa pamoja na Sheria ndogo  namba 2 ya 2015 ya uhujumu uchumi  .
Pia nashtakiwa  kwa mujibu wa Sheria  ya milipuko  kifungu cha Sheria namba 11(1) ikisomwa pamoja na Sheria namba 3 ya 2016
Pia alikuwa  nyara za Serikali  ukiwemo mkia wa nungunungu wenye thamani  ya Sh 336,000/-  na mikia miwili ya mnyama pori aitwae pongo  kwa jumla ikiwa na thmani ya Sh 1,344,000/-ikiwa nikinyume cha Sheria  namba 5  ya 2009 , kifungu cha 86(1) (2) (b) (II)
Swai aliamuru  mshtakiwa kurejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza  masharti ya dhamana  huku akiiahirisha  kesi hiyo hadi Desemba 22 , mwaka huu itakapotajwa tena .
Awali Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Baraka Hongoli alidai mahakamani hapo kuwa  mshtakiwa alitenda makosa hayo Desemba 03, mwaka  huu ndani ya Pori la Hifadhi la Rukwa – Lwafi  wilayani Mlele mkoani humo .
Mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa