Home » » WAWEKEZAJI MKOANI KATAVI WAOMBA KUBORESHWA KWA MIUNDO MBINU YA BARABARA.

WAWEKEZAJI MKOANI KATAVI WAOMBA KUBORESHWA KWA MIUNDO MBINU YA BARABARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Hapa wanasalimiana katia ya mku wa mkoa wa katavi na mkurugenzi wa GBP TZ
 Mkurugenzi wa GBP Tanzania Rashid Seif Soud  akimwelekeza mkuu wa mkoa wa katavi  Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga sehemu ya kukata utepe wake
 RC katavi akizindua kito kipya cha mafuta cha kampuni ya GBP Mpanda


 Na  Walter   Mguluchuma .
     Katavi.

Wawekezaji katika sekta ya mafuta mkoani katavi wameiomba serikali kulipatia ufunbuzi  changamoto ya miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa mafuta kutoka  Dares salam hadi mkoani Katavi  kufutia kujitokeza kwa wawekezaji wa mafuta kujenga vituo vya mafuta ambapo kampuni ya GBP imejenga kituo cha mafuta chenye thamani ya zaidiya milioni 500 Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na kupunguza adhaa ya upatikanaji wa mafuta katika mkoa huo wenye mahitaji kwa sasa kutokana na kuwa bado mkoa mchanga,

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha mafuta kinachomilikiwa na kampuni ya GBP ambaye ni mwekezaji kwenye sekta ya mafuta hapa nchini Mkurugenzi wa kampuni hiyo Rashidi Seif Soud ameleza kuwa chanagmoto ya miundo mbiu ya barabara katika mkoa huo bado ni changamoto kubwa,

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa pamoja na kuwepo changamoto wao kama wazao wa mkoa wa katavi wataendelea kuwekeza katika mkoa huo kwa kuwa kampuni ya GBP chimbuko lake ni Mpanda Mkoa ni Katavi. 

Amefafanua kuwa kampuni hiyo ambayo inamatawi yake karibu mikoa yote nchi ikiwa imejikitazaidi katika mikoa ya kanda ya ziwa na ukanda wa magharibi mikoa ya Mwanza ,Simiyu Geita,Kagera,Mara na Shinyanga,Vilevile inayo matawi Zanzibar,Dar,Arusha na Mbeya  pia  matawi  mengine yako katika mikoa ya Kigoma Tabora na Katavi pamoja na nchi ya jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC.

Aidha ameleza kuwa katika kutekeleza azma ya serikali ya awam ya tano ya  Dkt Pombe Magufuli ya Tanzania ya Viwanda  na kuzalisha ajira wao kama wawekezaji wameweza kuzalisha ajira zaidi ya 1000 hapa nchini na ni moja ya Kampuni ya Mafuta inayoongoza katika ulipaji wa kodi ambapo kwa miaka miwili mfulizo wamekuwa wakilipa kodi bila matatizo


Katika uzinduzi huo Mkurugenzi huyo ametoa mifuko 500 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa Katavi itakayosaidia katika ujenzi wa kiwanja cha michezo kilichoanza kujengwa Mwaka huu, na kilitumika katika uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa wakati wa uwashaji wake uliofanyika mwezi April 2 mwaka 2017.na sasa unaendelea kujengwa taratibu kwa ajili ya shughuli nyingine za michezo.

Hivyo kufunguliwa kwa kituo hicho kitasaidia kwa njia moja au nyingine kuwahuduamia wananchi na kitaongeza ajira kwa wananchi walio wengi hapa mkoani.


Akiongea katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amepongeza juhudi zilizochukuliwa na wawekezaji hao kuwekeza katika mkoa wa katavi,na kueleza kuwa hata wengine waige mfano huo kuliko kwa kuwa wapo wanakatavi wengi walioko nje ya mkoa wa katavi na uwezo wanao lakini hawataki kuja kuwekeza wanataka waletwe wakiwa wameisha kufa niyo waletweMpanda inakuwa haiana maana ni vyema wakaja kuwekeza wakiwa bado wako hai.


Akizungumzia miundo mbinu ya barabara amaesema serikali inaendelea kuhakikisha inatengeneza miundombinu hiyo ya barabara kwa kuwanza ujenzi wa lami katika baabara ya Mpanda Inyonga hadi Tabora inayoanza kujengwa mwezi ujao .

Pia serikali inaendelea kuhakkiisha inaboresha miundo mbinu ya barabara kwa kujenga kwa kiwango cha lami ambao barabara ya kutoka Mpanda Stalike kwa kiwango cha lami imekamilika na Sasa inaendelea kujengwa ya kutoka Mpanda kilometa 30 kuelekea mkoani kigoma wakati wakandarasi wengine wameanzia uvinza mkoani Kigoma kuelekea mpanda,juhudi zinaendeleakuhakikisha uimarishaji wa miundo mbinu hiyo inaimarika ili kukabiliana na changamoto hiyo hivyo wawekezaji wasiogope kuja kuwekeza katavi.
Akizungumzia ujenzi wa uwanja wa michezo amepongeza na kushukuru kwa msaada uliotolewa na Mkurugenzi wa GBP kutoa mifuko 500 ya saruji itakayosaidia katika ujenzi wa uwanja huo, akahimiza na wengine wajitokeze kuchangia chochote ili kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.

Pia akashukuru kwa njia moja au nyingie=ne wale waote waliojitolea kwa hali na mali katika ujenziwa uwanja huokuanzia wananchi wajasiliamali wafanyabiashara na makampuni pamoja na Taasisi   mbalimbali zikiwemo Halmashauri za wilaya  zilizoko mkoani hapa.

Wily Mbogo ni Meya wa Halmashauri ya Mpanda ameshukuru kwa uwekezaji mzuri kwa kuwekeza fursa nzuri ya kukuza uchumi pamoja na misaada ya mifuko 500 ya saruji na kisima kirefu cha maji kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Majengo Halmashauri ya Mpanda.
Nasoro Alfi ni Mwenyekiti wa Usafirishaji mkoa wa katavi amehimiza watumiaji wa vyombo vya moto kutumia kituo hicho kwa kuwa kitasaidia kwa njia moja au nyingine kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta unaokuwa unajitokeza mara kwa mara katika mkoa huo  wa Katavi,na watoe ushirikianao wa karibu.

Nao wananchi katika Mkoa wa Katavi  Fatuma Rashi na wamepongeza moyo ulioneshwa na mwekezaji na kueleza kuwa kuwepo kwa uwekezaji huo kutasaidia kuongeza ajira kwa vijana na huduma nzuri kwa watumiaji wa vyombo vya moto hivyo wamuunge mkoano na kumpatia ushirikiano mkubwa mwekezaji huyo.




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa