Home » » MARIE STOPES WATOA ELIMU KWA WANAFUNZI JUU YA AFYA YA MSINGI NA UZAZI WA MPANGO.

MARIE STOPES WATOA ELIMU KWA WANAFUNZI JUU YA AFYA YA MSINGI NA UZAZI WA MPANGO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


  Na   Walter  Mguluchuma.
               Katavi .
Shirika la  Marie  Stopes  Tanzania  ilimetowa   elimu kwa  Wanafunzi wa  Shule  kumi za   Sekondari za  Manispaa ya   Mpanda  ya juu ya     uzazi wa    mpango na  afya ya   msingi na  namna ya  kujikinga  na    maambukizi ya VVU.
 Shirika  hilo  lilitowa   elimu  hiyo wakati wa  kongamano la  situ tatu  ambapo  maadhimisho yake yalifanyika  jana katika  uwanja wa   shule ya   Msingi   Kashaulili  katika   Manispaa  ya   Mpanda    Mkoani  hapa .
Mratibu wa   Vijana   Marie   Stopes   Tanzania   Daniel   Mjema    Emanuel    alieleza kuwa  kongamano  hilo liliandaliwa na  shirika la   Marie    Stopes  Tanznia kwa kushirikiana  na   ofisi ya    Mganga  Mkuu wa   Mkoa wa  Katavi.
Alieleza kuwa   lengo la  kongamano  hilo la  siku  tatu  ilikuwa ni kutowa    elimu kwa   wanafunzi wa   shule za   sekondari na kwa   vijana ambao sio   wanafunzi   yenye  lengo la kuwapati  Afya ya  msingi,uzazi wa    mpango na   namna ya kujikinga  na  maambukizi ya VVU  pamoja na kujiepusha  na mimba  za utotoni .
Alisema  katika kongamano hilo  wametowa furusa  pia ya watu kujipima  na kutambua afya zao  na wameweza kutowa pia  elimu ya   afya ya   uzazi kwa watu mbalimbali waliofika kwenye kongamano hilo.
Nae   mratibu wa  Marie   Stopes  Mkoa wa   Katavi   Seif   Kijiko  alieleza  kuwa   Mkoa wa   Katavi  ni  miongoni mwa  mikoa   ambayo  inaongezeko  kubwa  la  mimba za utotoni kwa  wasichana   wenye   umri  mdogo .
Alifafanua  kuwa katika kukabiliana  na  tatizo  hilo la   mimba za utotoni  Marie  Stopes   wamekuwa wakitowa  elimu  mbali  mbali  kwenye   mashule ya   sekondari   na  katika   maeneo  yenye  mikusanyiko ya  watu  katika  maeneo yote ya   Mkoa wa   Katavi .
Kijiko   alisema   licha  ya  jitihada  hizo    zinazofanywa   na    shirika   hilo wamekuwa  wakikabiliana  na   changamoto  mbalimbali      na   alitaja   baadhi ya    changamoto   iliyopo   kuwa nia.
Baadhi ya   walimu wa   shule  za   Sekondari wamekuwa  wakikataa kutowa   ushirikiano kwa   Marie Stopes kwa kukataa   elimu ya   afya na   uzazi wa   mpango isitolewe  kwenye   shule  zao .
Kwa  upande  wake    Mraribu wa   afya  na   uzazi wa  mpango  wa  Manispaa ya  Mpanda  Muna  Sumry  alieleza  kuwa Manispaa ya   Mpanda  wameanza  kutowa   elimu  kwenye   shule za    msingi  juu ya   madhara ya kupata  mimba za utotoni ikiwa ni hatua  moja wapo ya kupunguza  tatizo la  mimba za  utotoni .
Mgeni   rasmi wa  kongamano  hilo  Kaimu    Katibu   Tawala wa  Mkoa  wa   Katavi   Willbard  Marandu   alieleeza kuwa  tatizo la wasichana kubeba  mimba wakiwa na umri mdogo umekuwa ukisababisha vifo vya mama na mtoto .
Alisema  imani  potofu  imekuwa ikichangia  watu kutofuata uzazi wa mpango  kwani wanaamini  kuwa mwanamke  ni chombo  cha  kuzaa watoto  hivyo  hari  hiyo  imekuwa isababbisha watu kuzaa  ovyo ovyo bila kufuata uzazi wa mpango na kuwa na familia kubwa  ambayo hushindwa kuitunza.
Velinaice  Godwin  Mwanafunzi wa  shule ya  Sekondari  ya  Wasichana   Mpanda    eleleza  kuwa   elimu walipatiwa na  Marie   Stopes    imewasaidia  sana kutambua   umuhimi wa   uzazi wa   mpango na jinsi ya kujiepusha na  mimba za utotoni na  kujikinga na maambukizi ya VVU.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa