Home » » WIZARA YA AFYA YAPANDISHA ZAHANATI KUWA HOSPITALI YA WILAYA

WIZARA YA AFYA YAPANDISHA ZAHANATI KUWA HOSPITALI YA WILAYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Na  Walter  Mguluchuma.
      Katavi .
 Waziri wa  Afya,Maendeleo  ya  Jamii ,  Jinsia   Wazee  na  Watoto   Ummy    Mwalimu  ameipandisha   hadhi  Zahanati ya  Inyonga  kuwa  Hospitali ya  Wilaya ya  Mlele  Mkoani    Katavi  baada ya kuikagua na  na  kuridhishwa na  sifa za kuifanya kuwa  Hospitali ya  Wilaya.
  Mwalimu  aliipandisha  Zahanati  hiyo  kuwa   hospitali ya  Wilaya   hapo   jana mara  baada ya    kuikagua  na   kuridhishw   na  vigezo   vinavyo   takiwa   vya    kuipandisha   hadhi  Zahanati  hiyo kuwa  Hospitali ya   Wilaya .
  Alisema      ameamua   kuipandisha   hadhi   zahanati  hiyo  kuwa    Hospitali ya   Wilaya   kutokana  na   mamlaka    aliyonayo    kama   Waziri wa   Wizara   husika.
  Alivitaja   baadhi ya   vigezo   vinavyofanya  Hospitali  iwe  na  hadhi ya  Hospitali ya   Wilaya  kuwa  ni  huduma  ya   upasuaji ,  Chumba  cha kuhifadhi  maiti ,  maabara ,  huduma ya  maji,umeme wa  uhakika  na    huduma ya   damu .
  Alifafanua  kuwa   kama   zahanati  hiyo  inatowa   huduma  kama   hospitali  ya   Wilaya kwanini  yeye  kama   Waziri  mwenye  dhamana  ashindwe  kuipandisha   hadhi   Zahanati   hiyo na   ukiangalia pia   Wilaya  hiyo  haina  Hospitali  hata  moja ya  Wilaya .
 Mwalimu   alisema   Rais  John  Magufuli  Alisha  waagiza   Mawaziri  kuwa  na    uamuzi wa  kutowa  maamuzi  magumu  pale   panavyositahili  kama  ambavyo    alivyofanya  yeye  kuipandisha   hadhi   Zahanati  hiyo kwani   .
Na   alitowa  ahadi ya kupeleka  wataalamu  wa   Afya  haraka   iwezekanavyo  wenye   hadhi ya    kufanya  kazi   kwenye   Hospitali  hiyo   haraka  iwezekanavyo   kabla  ya  mwezi wa  Septemba  hauja  kwisha .
  Waziri huyo   alikabidhi   kwa  niaba  ya  Rais  magodoro  20  na    ,vitanda  20      shuka  50 na  vitanda  vitano vya kisasa  vya kujifungulia  akina  mama wajawazito kwa  kwa   ajiri ya      Hospitali  hiyo ya  Wilaya.
Nae   Mganga   Mkuu  wa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mlele  DR    Luccy  Kafumu   alieleza  kuwa   mchakato  wa  maombi wa  kuipandisha   hadhi   zahanati  hiyo  ulianza  toka  mwaka  2013  baada ya wao  kuona  inasitahili kuwa  Hospitali ya   Wilaya .
  Dr   Kafumu  alieleza  kuwa  Zahanati  hiyo  kwa  muda  wote toka  mwaka  2013  imekuwa  itowa  huduma   kama   Hospitali ya  Wilaya  kwa   kitendo  hicho   cha   kuipandisha   hadhi   kitasaidia  hata  hela za kununua  dawa  kuongezeka  kwenye  bajeti  ijayo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa