Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mejagenerali mstaafu Raphael Muhuga ameiomba Serikali kuwaondoka na kuwapeleke kwenye kambi za Wakimbizi Raia wa Nchi ya Burundi na Kongo ambao wananchi kwenye Makazi ya Wakimbizi ya Mishamo na Katumba Mkoani Katavi ambao mpaka sasa hawaja pata urai wa Tanzania .
Muhuga alitowa ombi hilo hapo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Anjelina Mabula wakati alipokuwa akimsomea taarifa ya Mkoa wa Katavi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi .
Alisema Mkoa wa Katavi unazo kambi mbili za wakimbizi katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba na Mishamo ambapo wakimbizi 15,0000 hawajapewa Urai wa Nchi hii huku asilimia 90 ya raia hao waliokuwa raia wa Nchi ya Burundi wakiwa wamepewa Urai wa Tanzania .
Alieleza kuwa Raia hao wa Nchi jirani kuendelea kuwepo kwenye kambi hizo bila kuondolewa na kupelekwa kwenye kambi nyingine kumekuwa kukisababisha hata wale waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi na kupewa urai wa Tanzania kutotii maagizo yanayo kuwa yanatolewa na Viongozi wa Serikali wa Mkoa na Wilaya .
Alifafanua kuwa watu wanaoishi kwenye Makambi hayo wamekuwa wakiwatii zaidi wakuu wao wa Makazi ya Katumba na Mishamo kuliko yeye Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya zilizoko kwenye kambi hizo ambazo ni Wilaya ya Mpanda na Wilaya mpya ya Tanganyika .
Muhuga alieleza kuwa Serikali imewapatia urai zaidi ya watu laki moja wanaishi kwenye makazi hayo na kabla ya kupewa urai watu hao walikuwa wakihudumiwa na shirika la wakimbizi UNHCR ammbao sasa hivi wameacha kuwahudumia watu hao .
Kutona na UNHCR kuwacha kutowa huduma kwa watu hao wamekuwa wakipata shida kupata huduma muhimu hivyo ni vema Serikali ikatangaza kuyafunga makambi hayo rasmi ili watu hao wapatiwe huduma na serikali .
Kwani kwa sasa hata wanapotewa maelekezo ya kufanya shughuli za Maendeleo wamekuwa hawatii mpaka waagizwe na Mkuu wao wa Makazi si Mkuu wa Mkoa wa mkuu wa Wilaya.
Makazi ya wakimbizi za Mishamo iliyoko katika Wilaya ya Tanganyika na makazi ya Katumba iliyoko Wilaya ya Mpanda zilianzishwa mwaka 1972 baada ya kutokea kwa vita Nchini Burundi
MWISHO
0 comments:
Post a Comment