Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anjela Mabula ametowa wito kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi kununua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa zilizopo katika maeneo ya Halmashauri zao ilikupunguza tatizo la nyumba za makazi ya watumishi wao .
Naibu Waziri huyo alitowa wito huo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mkoa wa Katavi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani hapa ya lengo la kusikiliza kero mbalimbali za migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Katavi .
Alisema shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba nyingi katika Mkoa wa Katavi hivyo ni vema Halmashauri za Mkoa huo zikatumia furusa hiyo kwa kuzinunua nyumba hizo kwa ajiri ya watumishi wao .
Alieleza kuwa shirika hilo limeanzisha mpango mpya wa kununua nyumba za shirika hilo unaoitwa mpamgaji mnunuzi ambao unampa nafasi mtu mwenye kipato kidigo kununua nyumba za NHC.
Katika mpango huo mpangaji atalipa asilimia 25 ya bei ya thamani ya kununulia nyumba na kisha atakaa kwenye nyumba hiyo bure kwa kipindi cha miezi mitatu na baada ya hapo ataanza kulipia kodi ya nyumba ambapo kodi hiyo atakayo kuwa analipia ikifikia thamani ya bei ya kuuzia nyumba nyumba hiyo inakuwa ni mali ya mpangaji huyo .
Pia Anjela Mabula aliliagiza shirika la NHC kufanya msako kwenye vikundi vya vijana ambao walipewa mashine za kufyatulia matofali na vikundi ambavyo vitabainika mashine walizopewa na shirika hilo na hazifanyi kazi basi vikundi hivyo vinya ng-anywe na kupewa vikundi vingine vya vijana .
Pia aliziagiza Halmashauri za Mkoa wa Katavi kuhakikisha zinaweka mipaka ya vijiji kwenye maeneo yao yote ili kuepusha migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara kutokana na kutokuwepo kwa mipaka.
Aliziagiza Halmashauri za Mkoa wa Katavi kuhakikisha zinapima maeneo ya mikapa ya kila Kijiji ili kuondokana na migogoro ya ardhi na aliziagiza zifanye hivyo katika kipindi kisicho zidi miezi mitatu kuanzia sasa .
Meneja wa NHC George Magembe alisema shirika hilo limejenga nyumba 95 katika Mkoa wa Katavi katika Wilaya za Mpanda na Mlele .
Alifafanua nyumba 70 zimejengwa katika Manispaa ya Mpanda katika eneo la Ilembo na zimegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 ambapo hadi sasa ni nyumba sita tuu ambazo zinawapangaji huku nyumba 63 zikiwa zimekaa bila wapangaji pia NHC inajenga jingo la kitega uchumi katika eneo la Paradise katika manispaa hiyo ya ghorofa nne na ujenzi wake utakapo kamilika utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3.5.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele shirika hilo linajenga nyumba 24 na wanatarajia kuanza ujenzi wa mradi mwingine wa kujenga nyumba 18 za Walimu katika shule ya Msingi ya Kakuni katika Halmashauri ya Mpimbwe .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment