Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inafanya uhakiki wa kuvibaini vikundi vyote vya Vijana na Wanawake kwa lengo la kuvibaini vikundi hewa ambavyo vimekuwa vikijipatia mikopo inayotolewa na Halmashauri hiyo .
Hayo yalisemwa hapo jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji .
Alisema kumekuwepo na tabia kwenye Halmashauri hiyo kwa vikundi vya Vijana na Wanawake vinavyokokeshwa fedha iliyotengwa kutokana na asilimia tano ya mapato ya ndani kwa vikundi vichache kuwa vina jirudia kila mwaka kupata mkopo wakati takwimu zinakuwa zinaonyesha kuwepo kwa idadi kubwa ya vikundi huku wanufaika vikiwa ni vikundi vilevile kila mwaka .
Mapengo alilieleza Baraza hilo kuwa kutokana na hari hiyo ndio maana Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ameanza kufanya kazi ya kuvihakiki vikundi vyote vilivyo sajiriwa vya vijana na wanawake ili kuvibaini vikundi hewa vyote vilivyopo kwenye Halmashauri hiyo watu wasidhani kuwa Nchi hii inawatumishi hewa tuu na mishahara hewa bali pia hata vikundi vipo ambavyo ni hewa .
Mwenyekiti huyo ambae ni Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo aliwaonya madiwani wenzake waache tabia ya kuvizua vikundi kurejesha fedha wanazokuwa wamekopeshwa na Halmashauri hiyo kwa lengo la kujitengenezea siasa kufanya hivyo ni kuwadanganya wananchi wao kwani fedha hizo n lazima zirudishwe ili ziendelee kutolewa kwa vikundi vingine .
Alisema katika mwaka huu wa fedha wa 2016 na 2017 Halmashauri hiyo tayari imeisha tenga kiasi cha shilingi milioni sabini kwa ajiri ya kuvikopesha vikundi vya Vijana na Wanawake .
Nae Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mpanda Bi Halma Kitumba alilieleza Baraza hilo la Madiwani kuwa wamepanga kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani watu wote ambao walichukua mikopo hiyo na hawajazirejesha .
Alisema wameisha waagiza kuwa ifikapo Oktoba 17 vikundi vyote viwe vimerejesha fedha walizokopesha na wale watakao shindwa wataanza kukamatwa kuanzia siku hiyo ambapo hadi sasa tayari wamekusanya kiasi cha Tsh 123,000,000.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso alieleza endapo fedha hizo zinazotolewa na Halmashauri hiyo na zitasimamiwa vizuri kwenye vikundi malengo na dhamira ya Serikali itaonekana katika mpango wake wa kuwasaidia Vijana na Wanawake .
Alisema Madiwani wanayonafasi kubwa ya kuwaelimisha Wananchi kwenye Kata zao kuwa fedha hizo zinazotolewa kwenye vikundi sio fedha za sadaka bali zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kisha kurejeshwa kwenye Halmshauri .
Alifafanua kuwa makundi mengi ya vijana hayaja kiweke kwenye makundi wanaojiunga ni Wanawake ambao nao vikundi hivyo vimekuwa haviendelei.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment