Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Zaidi ya Wanawake 270 wamefariki Dunia Mkoani Katavi mwaka 2015 kutokana na vifo vilivyo tokana na matatizo ya uzazi kwa kila vizazi hai 100,000 idadi hii ya vifo ni kwa wale waliotolewa taarifa zao.
Hayo yalisemwa hapo jana na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Obed Mahenge wakati wa tamasha kubwa la Vijana lililowashirikisha pia wanafunzi wa shule za Sekondari na chuo cha VETA Mpanda tamasha hilo ilililoandaliwa kwa lengo la kutowa elimu kuhusu uzazi wa Mpango lililoandaliwa na Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na fisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda .
Alisema katika Mkoa wa Katavi kiwango cha vifo vya Wanawake vilivyo tokea katika kipindi cha mwaka jana kutokana na matatizo ya uzazi ni wanawake 277 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa ,idadi hii ni kwa wale ambao taarifa zao zilitolewa .
Kiwango cha utumiaji wa njia za uzazi wa mpango katika Mkoa wa Katavi kwa mwaka jana ilikuwa ni asilimia 41.1 tu kiwango hiki kiko chini sana kikilinganishwa na kiwango cha Taifa cha asilimia 60.
Aidha imani potofu na taarifa zisizo sahihi kuhusu uzazi wa mpango zimesababisha kina Mama wengi kuwa waoga wa kutumia njia hizi na kuishia kushika mimba zisizotarajiwa .
Alisema kuwa Wanawake wana haki ya kutumia njia ya uzazi wa mpango kwa ajiri ya afya zao na familia kwa ujumla hivyo alitowa wito kwa wanaume wa Mkoa wa Katavi kuwa bega kwa bega na wake zao katika kutumia njia za uzazi wa mpango kwani mwisho wa siku watafaidika wote kwa kuwa na familia yenye afya bora .
Mratibu wa Marie Stopes Tanzania wa Kanda ya Nyanda za juu kusini Noelia Mbeyela alisema wanawake wengi hapa Nchini wamekuwa wakipata mimba za utotoni huku wakiwa na umri wa chini ya miaka 19 kitu ambacho ni hatari kwa afya zao.
Alisema kitendo hicho cha wasichana kupata mimba wakiwa na umri mdogo kimekuwa kikiwasababishia kupoteza maisha yao wakati wa kujifungua na kupata maambuzi ya VVU kutokana na kutojua kujikinga na maambukizi ya VVU kwa ajiri ya kuwa na umri mdogo.
Mbeyela alieleza kitendo hicho cha kubeba mimba wakati wakiwa bado wadogo kimekuwa pia kikiwasababishia kushindwa kuendelea na masomo kwani umri huo wa miaka 19 ni msichana kuwa shule .
Alisema ushiriki wa wanaume kwenye maswala ya mpango wa uzazi ni mdogo sana swala hilo linaonekana ni kama vile na wanawake peke yao hivyo wanaume wajenge tabia ya kufuatana na wake zao kwenye maeneo ambayo elimu ya uzazi wa mpango inapokuwa ikitolewa .
Athari nyingine ya kuzaa wakiwa na mri mdogo aliitaja kuwa ni msichana kuchukua jukumu la kuanza kulea familia wakati ajafikia umri w a kutunza familia matokeo yake imekuwa ikiathiri uchumi wa Nchi kwa Nchi kuwa na wategemezi wengi .
Mratibu wa Marie Stopes wa Mkoa wa Katavi Seif Mjuni alisema elimu ya uzazi wa mpango katika Mkoa wa Katavi ilichelewa kuwafikia wananchi wa Mkoa huo na ndio maana unakabiliwa na tatizo kubwa la mimba za utotoni kwa wasichana .
Alisema wapo watu wanaamini kuwa kuzaa watoto wengi ni utajiri na wapo wanaoamini kuwa mwanamke ni chombo cha kuzaa tuu
Aidha imani potofu na taarifa zisizo sahihi kuhusu uzazi wa mpango zimesababisha kina mama wengi kuwa waoga wa kutumia njia hizi na kuishia kushika mimba zisizotarajiwa .
Kwa kutambua hilo Marie Stopes Tanzania imeanza kutow elimu ya afya ya uzazi wa mpango katika maeneo yote ya Halmashauri za Mkoa wa Katavi kwa kuwaelisha faida za kufuata uzazi wa mpango na kujikinga na maambukizi ya VVU na madhara ya mimba za utotoni
Nae Makamu Meya wa Manispaa ya Mpanda Kanoni Lucas alisema kasi ya ongezeko la watu Tanzania ni kubwa sana ukilinganisha na kasi ya ukuaji wa uchumi wetu na hivyo tusipozaa watoto tunao weza kuwasomesha tutakuwa tunatengeneza Taifa la watu dhaifu katika ushiriki wa shughuli za maendeleo na hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia .
Aliipongeza Marie Stopes Tanzania pamoja na Taasisi zote ambazo ni wadau katika kuhamasisha na kutowa huduma za uzazi wa mpango kwa kuonyesha ushirikiano kwa Serikali.
Alisema kupitia Marie Stopes Tanzania na taasisi nyingine huduma za uzazi wa mpango hususani huduma rafiki kwa vijana zimepelekwa karibu zaidi na wananchi hivyo afya za wananchi zitaboreka na hatimae kuleta maendeleo ya Mkoa wa Katavi na Taifa kwa ujumla .
Katika tamasha hilo ambalo lilihudhuliwa na watu wengi wa lika mbalimbali pia huduma ya upimaji wa VVU ilitolewa katika mabanda yaliokuwa yameandaliwa pamoja na elimu ya uzazi wa mpango
0 comments:
Post a Comment