Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Katavi
SERIKALI ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imewaagiza
maofisa ugani kuwaelimisha wananchi ili waweze kufanya mageuzi
mageuzi ya kilimo chenye tija kwa kulima mazaomengine ya biashara
badala ya kutegemea zao moja tu la tumbaku .
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi ,
Salehe Mhando wakti alipokuwa akizungumza na watumishi wa wilaya
yake , akisisitiza kuwa wakati sasa umewadia kwa wakulima wilayani
humo kuanza kulima mazao ya kahawa na ufuta kama mazao ya
biashara badala ya kutegemea zao moja la tumbaku .
“Wakulima wetu wanalima zao la tumbaku kama zao la biashara pia
mahindi kwa ajili ya chakula na kama zao la biashara ….. hali ya
hewa ya wilaya hii haitofautiani na ile ya mikoa inayostawisha
ufuta na kahawa kwa wingi
….. hivyo ni vema maofisa ugani wetu wakaanza kuwahamasisha kulima
ufuta na kahawa ili kupanua wigo wa mazao ya biashara ambayo
yaataongeza kipato kwa mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla wake
“ alisisitiza.
Aliwaeleza watumishi hao kuwa Serikali ya Wilaya ya Tanganyika
imejipanga kutekeleza ahadi za miradi ya maendeleo zilizomo
katika Ilani ya Uchaguzi zilizohaidiwa wakati wa Kampeni za
Uchaguzi Mkuu uliopita na zilizotolewa ambazo haziko kwenye
Irani hiyo ..
Alisema jamii imebadilika inataka kushuhudia vitendo na sio
porojo akiwatak maofisa mipango wafanye kazi kwa vitendo ili
kuhakikisha kuwa wilaya hiyo inakuwa na vipao mbele vyake .
Alizianisha changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na
uhaba wa maji safi na salama , upungufu wa vituo vya afya vilivyopo
ni vitatu huku kata zikiwa 16 pia uhaba wa vyumba vya madarasa kwa
shule za msingi ambapo wanafunzi wanalazimika kusomea nje huku
akisisitiza kuwa lazima kila shule ihakikishe inajenga vyumba vya
madarasa vinne hadi ifikapo Desemba mwaka huu ..
Alisema kwa upande wa shule za Sekondari zipo kata sita
ambzo hazina shule za Sekondari huku mpango wa serikali
ukisisitiza kila Kata ijenge shule moja ya sekondari .
Aidha ameziagiza Idara za ushirika naIdara ya Maendeleo ya
Jamii kufanya kazi kwa kushirikiana kwa kuwahamasisha vijana
kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mkopo wa asilimia tano
zinazotolewa na halmashauri hiyo .
0 comments:
Post a Comment