Home » » MKUU WA WILAYA AAGIZA KILA KIJANA KULIMA HEKARI MBILI IFIKAPO MSIMU UJAO WA KILIMO

MKUU WA WILAYA AAGIZA KILA KIJANA KULIMA HEKARI MBILI IFIKAPO MSIMU UJAO WA KILIMO



Na  Walter  Mguluchuma
 Katavi
Mkuu wa wilaya ya mlele mkoani Katavi Rachael Kasanda amewaagiza vijana wote waliopo wilayani humo kuhakikisha msimu ujao wa kilimo kila kijana analima shamba lenye ukubwa wa hekari mbili zitakazo wawezesha kipata kipato mara baada ya mavuno.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara wilayani humo alisema vijana wangi wamekuwa hawajishughulishi katika shughuli za kilimo badala yake wamewaachia wazazi wao na wao kuishia wakiponda raha vijiweni.
Kasanda alisema kuwa huu si wakati wa kuwavumilia vijana hao kwani ndio wanaosababisha usumbufu katika jamii kwani wanamahitaji ya kipato na kwakuwa hawafanyi kazi wanaishia kwenye wizi na matendo mengine yasiyo faa.
Alisema kutokana na hali hiyo amewaagiza viongozi wa serikali za mitaa kuwabana vijana hao katika msimu wa kilimo ujao ili walime walau kila kijana hekari mbili ambazo Zitawapatia kipato hapo baadae baada ya kuvuna.
Pia alitoa wito kwa wakulima wa wilaya hiyo kujituma katika msimu ujao wa kilimo kwa kulima huku wakizingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa tija na kuja kunufaika na mazao watakayo yapata.
Aidha mkuu huyo wa wilaya pia aliwakumbusha watumishi wa umma wilayani humo kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi kwani utendaji wa hovyo wa baadhi ya watumishi ndio chanzo cha wananchi kuitukana serikali yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa