Home » » HOT: WATU WAWILI JELA MIAKA 40 KWA KOSA LA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO MSHITAKIWA ABANWA NA AJA NDOGO NA KUTOKWA NA JASHO JINGI WAKATI AKISOMEWA HUKUMU .

HOT: WATU WAWILI JELA MIAKA 40 KWA KOSA LA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO MSHITAKIWA ABANWA NA AJA NDOGO NA KUTOKWA NA JASHO JINGI WAKATI AKISOMEWA HUKUMU .


       Na  Walter    Mguluchuma .
                 Katavi .
  Mahakama  ya   Wilaya   Wilaya ya  Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  imewahukumu    Watu   wawili   Nzira   Luhemeja   42  na   Vicenti  Makelele      32  wakazi  wa   Kijiji  cha  Mwamkulu  Wilaya ya  Mpanda  jumla ya  kifungo  cha miaka    40  jela  baada ya kupatikana  na  hatia  ya  kukamatwa  na   nyama ya  kiboko  kilo  70 wakiwa  ndani ya  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi .
Hukumu  hiyo  ilitolewa  hapo   leo   na  Hakimu   Mkazi  wa  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda    Odira  Amwol  baada ya  Mahaama  kulidhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo  na  upande wa  mashitaka  uliokuwa    unaongozwa  na Elieza   Chitalya    mwendesha  mashitaka wa TANAPA ulikuwa na  mashahidi wane na washitakiwa  walijitetea  wenyewe.
 Wakati wa usomaji wa  hukumu  hiyo   Mahakama  iliazimika  kusimama kwa  muda  wa  dakika  kumi baada  ya  mshitakiwa  wa    kwanza   Nzira   Luhemeja  kubanwa  na  aja   ndogo na  kutokwa  na jasho  jingi   wakati wakisomewa  hukumu ya  kesi  hiyo na    Hakimu  Amwol.
 Na  ililazimika    apelekwe  chooni  kwenye  choo cha   Mahakamani  hapo  na  Askari  polisi  na  kisha   alirudishwa  kizimbani na  Mahakama  iliendelea.
Awali  katika  kesi  hiyo   mwendesha   mashitaka  wa   TANAPA  alidai kuwa  washitakiwa  hao  walikamatwa  hapo  Julai  21  mwaka  huu  huko   katika   eneo  la   Mto   Katuma   ndani ya   Hifadhi  ya  Taifa    ya  Katavi .
   Chitalya   alidai kuwa  washitakiwa  hao  wote  wawili kwa  pamoja  walikamatwa   katika   eneo  hilo  na   Askari wa  Hifadhi ya   Katavi  walikuwa  dolia  na waliwakamata wakiwa  na  nyama ya  Kiboko  yenye  uzito  wa  kilo   70  yenye  thamani ya  shilingi  milioni  tatu  .
Ilielezwa  Mahakamani  hapo    washitakiwa  hao walikamatwa  wakiwa na mguu  mmoja wa    Mnyama  Kiboko    ambapo ni sawa  na  Kiboko  mmoja   ambae  yuko  hai   wakiwa  wamepatikia  kwenye    mfuko wa   sandarusi na wakiwa na    baiskeli  mbili .
Katika  utetezi  wao   mshitakiwa  wa  kwanza   Nzira   Luhameja   alikana  kukamatwa  na   nyara  hizo za   serikali   bali   alidai kuwa  yeye   alikamatwa  wakati  akiwa  njiani   anakwenda kuoga   katika  mto  Mafunsi  ambao  upo   nje ya    Hifadhi ya  Katavi  na  wala  hakuwa  na  nyara  hizo  za   Serikali.
Na   mshitakiwa  wa  pili yeye   alidai kuwa  yeye   hakukamatwa na  nyama   hiyo ya  Kiboko  bali    Askari wa  Tanapa  walimkamata  wakati   akiwa njiani  anaelekea  kuvua  samaki   katika  mto  Mafunsi.
Kabla  ya   Hakimu  Odira  Amwol  haja  towa    hukumu  hiyo   mwendesha  mashitaka wa  TANAPA  Elieza  Chitalya   aliiomba     Mahakama   hiyo  itowe  adhabu kwa  washitakiwa  hao  kwa  mujibu wa  sheria ya kosa walilopatikana  nalo  ili  iwefundisho kwa   jamii  nyingine .
Kabla ya  kutowa   adhabu kwa  washitakiwa    Hakimu    Amwol  aliwapa  nafasi washitakiwa   na  aliwaeleza   kama  wanayo  sababu  yoyote ya  msingi  yakuishawishi  mahakama iwapunguzie   adhabu wanayo   nafasi ya kujitetea .
Katika    ombi  lake la    mshitakiwa  wa kwanza  aliomba  Mahakama  imwachie  huru kwani  yeye  hakutenda   kosa  hilo  bali   alisingiziwa tuu  na   Askari wa  Tanapa   hata   majirani  zake  wanajua  yeye   hana   tabia   hiyo .
Mshitakiwa  wapili yeye   aliiomba   Mahakama   isimpe   dhabu ya  kifungo    bali   impe  adhabu ya kulipa  faiini kwani  kuna   famila   ambayo inamtegemea  yeye ambao ni  mama   yake    mzaz ambae ni mzee  sana i  na   pia  ana  watoto .
Baada ya Mahakama  kusiliza  pande  zote  mbili za  mashitaka   na  utetezi   Hakimu   Mkazi   Odira   Amwol  alisoma  hukumu na  kuiambia  Mahakama  kuwa  washitakiwa   wote   wawili   Mahakama  imewahukumu     kutumikia   kifungo  cha  miaka   20  jela    kila  mmoja kuanzia  jana    na  kama  hawaja  ridhika  na   hukumu  hiyo  wanayo   nafasi ya kukata  rufaa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa