Home » » ALLY MWIZI JELA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMLAWITI MSICHANA MAKABURINI JUU YA KABURI.

ALLY MWIZI JELA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMLAWITI MSICHANA MAKABURINI JUU YA KABURI.


  Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
Mahakama ya  Wilaya ya   Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  imemuhukumu   Ally  Rashid    maarufu  Ally   Mwizi kifungo  cha  miaka   30  baada  ya  kupatikana  na  hatia  ya  kumlawiti  i kwa  nguvu  makaburini juu ya  kabur i   msichana  25 jina  limehifadhiwa  Mkazi wa Mtaa  wa  Kotazi  Mjini.
Hukumu  hiyo  iliyovutiwa  hisia  za  watu   wengi wa    Manispaa  ya   Mpanda     ilitolewa  hapo jana na   Hakimu   Mkazi     mfawidhi wa  Mahakama  ya   Wilaya  ya   Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada  ya  Mahakama  kulidhika  na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo    na  upande wa   mashitaka  ulikuwa  ukiongozwa  na  Mwanasheria  wa  Serikali  wa  Mkoa wa   Katavi   Jamila   Mziray .
Awali  katika  kesi  hiyo  mwandesha   mashitaka  mwanasheria  wa   Serikali  wa  Mkoa wa  Katavi   Jamila  Mziray  alidai     mahakamani  hapo  kuwa  mshitakiwa   Ally  Mwizi     alitenda  kosa  hilo  hapo   hapo   june  17  mwaka huu  majira ya saa    mbili  usiku  huko  katika  Makaburi ya   Kashaulili  yalioko  katika  mtaa wa  Kotazi  Mjini   hapa .
Ilidaiwa  kuwa  mshitakiwa kabla  ya kutenda  kosa  hilo  alimfuata   msichana  huyo  ambae   alikuwa   ameibiwa   vitu  vyake   vya   ndani ya  nyumba  hivyo  alimdanganya  kuwa  yeye   Ally   Mwizi   anaouwezo  wa  kumsaidia  kuvipata  vitu  vyake   vilivyoibiwa .
  Mziray  aliiambia   Mahakama  kuwa    baada  ya  msichana  huyo  kuahidiwa   na  mshitakiwa    kuwa  vitu  vyake  alivyoibiwa   vitapatikana   aliambiwa   amlipe  ujira  Ally   Mwizi   kiasi  cha   Tsh  30.000  ili   aende  akamwonyeshe  vitu  vyake    alivyoibiwa  na  alifanya  hivyo.
Ndipo   siku  hiyo ya  tukio  mshitakiwa  alimpigia  simu   msichana   huyo   majira  ya saa   mbili   ili  aweze  kumpeleka     kwenda  kumwonyesha  vitu   hivyo   alivyoibiwa .
Mziray  alieleza  baada  ya kuwa  amempigia  simu   mshitakiwa   alikwenda  nyumbani  kwa  msichana  huyo na  kumchukua  na  kisha   alikwenda  nae   kwenye  makaburi ya  Kashaulili kwa  lengo la  kwenda  kumwonyesha  vitu  alivyoibiwa  lakini  baada  ya  kufika  makaburini  mshitakiwa alipiga     ngwala  msichana  huyo na  kisha   alianza  kumlawiti  juu ya  kaburi  huku  akimtishia kumuuwa  endapo   angepiga  kelele .
Baada  ya  kumaliza  haja  yake   mshitakiwa   alimwomba  dada  huyo waende  kwenye  nyumba ya kulala   wageni  inayoitwa   Kingi   Parisi ili  wakaendelee  kufanya  mapenzi  zaidi ya     kwa  kile  alichodai   kuwa   eneo la   Kingi  Parisi  panafaa  zaidi  kufanyia  tendo la  ndoa kuliko juu ya  kaburi.
Aliiambia   Mahakama   ndipo  msichana  huyo   alipoamua  kupiga  mayowe   ya kuomba  msaada  na  watu  walifika  kwenye   eneo  hilo  na   waliweza  kumkamata   mshitakiwa .
Hakimu  MKazi   Chiganga  Ntengwa    akisoma  hukumu  hiyo    aliambia   mahakama   kuwa  kutokana  na   ushahidi  uliotolewa   Mahakama   hapo  pasipo   shaka  yoyote  mahakama  imemwona     Mshitakiwa   Ally    Mwizi  kuwa  amepatikana  na  hatia  ya   kifungu  cha   sheria   Namba  154  kidogo  cha kwanza  ya  makosa  ya   adhabu   sura  na    16.
Hivyo  kutokana  na  kupatikana  na  kosa  hilo  Mahakama  imemuhukumu  Ally   Mwizi  kutumikia  kifungo  cha  miaka    30  jela    ili  akitoka   gerezani   awe  na  tabia   njema  kwenye jamii  ya  watu .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa