Home » » WATU WANNE JELA MIAKA 60 KWA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO YA ZAIDI YA TSH MILIONI 371

WATU WANNE JELA MIAKA 60 KWA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO YA ZAIDI YA TSH MILIONI 371


  Na  Walter   Nguluchuma  .
          Katavi
  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda   Mkoa  wa   Katavi  imewawahukumu  watu  wane kifungo  cha   jumla ya  miaka   60  jela  baada ya  kupatikana  na  hatia  ya kukamatwa na  meno ya   Tembo  vipande  25  vyenye  uzito wa  kilogramu   46 ya  thamani ya Tsh  Milioni 371,600,000
Hukumu  hiyo  ilitolewa  hapo  jana  na  Hakimu  Mkazi     mfawidhi wa  Mahakama   ya  Wilaya  ya  Mpanda   Chiganga  Ntengwa   baada ya  Mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa   na   upande wa  mashitaka .
 Washitakiwa  waliohukumiwa kifungo  hicho   ni    Justine   Baruti    39   Mkazi  wa   Kijiji  cha    Ivungwe     Makazi ya   Katumba  Wilaya ya  Mpanda, Bonifaphace   Hoza   40 ,  Elias  Hoza   46 wakazi wa  Kijiji  cha   Kalela  Kasulu  Mkoa  wa  Kigoma  na   Credo   Gervas  45   Mkazi wa  Kijiji  cha  Ndurumo   Makazi ya  Wakimbizi ya  Katumba .
Katika  kesi  hiyo upande wa  mashitaka  uliongozwa na  wakili  wa   Seriali wa  Mkoa wa  Katavi  Wakyo   Simoni  na  ulikuwa  na   mashahidi  15  na  washitakiwa  walikuwa  wakitetewa  na  wakili    Elias  Kifunda  na  washitakiwa  hawakuwa na  mashahidi wowote  zaidi yao .
 Awali  katika  kesi  hiyo   mwendesha  mashitaka  mwanasheria  wa  serikali   Wakyo   Simo alidai  mahakamani  hapo  kuwa  washitakiwa  hao  walitenda  kosa  hilo  hapo   Desemba  24   2014   huko  katika   stendi kuu ya  mabasi  yaendayo  Mikoani  katika   Mtaa wa  Mji  mwema  Manispaa ya  Mpanda .
  Ilidaiwa  na   Mwendesha  mashitaka  huyo kuwa  siku  hiyo  ya  tukio  Askari wa  Hifadhi ya  Taifa  ya  Katavi na  Askari   polisi walipata  taarifa kutoka  kwa  raia  wema  kuwa  washitakiwa  hao   wamepanga  kusafirisha  meno ya   Tembo  kuyatoa   Mpanda na    kuyapeleka   Mkoani  Kigoma  kwa  kutumia  basi la  Kampuni  ya  Adventure  Connection  Bus.

 AliIambia  Mahakama    kufuatia  tarifa  hizo   Askari wa  Tanapa  na  Polisi walifika  kwenye  eneo  hilo la  stendi ya    mabasi  ambapo waliweza  kuwashika washitakiwa  wakiwa  na  meno  hayo  ya  Tembo   vipande   46  ndani ya   basi la  Kampuni ya  Adventure
Mwanasheria  huyo  alidai kuwa   mshitakiwa wa kwanza   Justine  Baruti siku  hiyo ya tukio   alishikwa  na  meno ya  Tembo  vipande 18  vyenye uzito wa kilogramu 33 yenye thamani ya Tsh milioni 249,600,000 na  mshitakiwa wa pili  Boniphace Hoza  alishikwa na  Meno ya Tembo  vipande  7 yenye uzito wa  kilogramu  13 yenye   thamani ya  Tsh  milioni  124,000,000 wakiwa wameyapakia kwenye basi la  Kampuni ya  Adventure  Connection.
 Akisoma  hukumu  hiyo  hapo jana   Hakimu  Chiganga  Ntengwa  alisema  mahakama  pasipo  mashaka  yoyote  imewaona  washitakiwa  wanayo   makosa  yaliyowatia  hatiani  kulingana  na ushahidi uliotolewa  Mahakamani  hapo .
  Hivyo   watuhumiwa  wa  kwanza  hadi  wane  Mahakama  imewahukumu  kifungo cha  miaka  mitano jela  kwa kila mmoja  kwa  kosa   la kuhusika  kuhujumu  uchumi  na  mshitakiwa wa kwanza  Justine   Baruti na  mshitakiwa  wa pili   Boniphace  Hoza  walihukumi  tena  kila   mmoja kifungo  cha  miaka  20  jela  kwa kosa  la kupatika  na  nyara za  serikali  na   adhabu  hizo zinakwenda kwa wakati mmoja .
  Mahakama  hiyo  pia  ilimwachia  huru  mshitakiwa wa  tano  Sadock  Masamba  katika  kesi  hiyo  baada ya  upande   wa  mashita  kushindwa  kutowa  ushahidi wa wa kumtia  hatiani  mshitakiwa . 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa